Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Goodluck Charles.

Wateja wa Tigo katika mikoa ya Lindi na Mtwara hivi sasa wanaweza kufurahia kuunganishwa na intaneti ya kasi kufuatia kampuni hiyo kupanua huduma yake ya 4G LTE katika miji hiyo ya kusini mwa Tanzania. Teknolojia ya 4G LTE ni ya kasi takribani mara tano zaidi ya teknolojia ya 3G iliyopo katika soko kwa hivi sasa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Goodluck Charles upanuzi huo unafuatia kuzinduliwa kwa mafanikio kwa huduma hiyo katika miji mingine 14 nchini.

Charles anasema “Kupatikana kwa teknoplojia ya 4G katika mikoa ya Lindi na Mtwara kunaonesha kuwa Tigo kwa mara nyingine jinsi ilivyojikita katika kuboresha mabadiliko katika mtindo wa maisha ya kidijitali na kuongoza kwake katika kutoa teknolojia ya kisasa na ubunifu ndani ya soko.”

Huduma ya 4G LTE inamaanisha kurambaza kwa kasi kubwa, kupakua vitu kutoka katika intaneti na kufanya miito ya mawasiliano ya simu kwa kuonana (skype). Hali kadhalika inawezesha wateja kwa kiwango kikubwa kutiririsha video na hata mikutano ya video. Hali kadhalika na matumizi mengi kama vile kufanya mkutano kwa video, ubora wa hali ya juu, blogu za video michezo na kupakua video kutoka kwenye mitandao ya jamii.

Mtwara na Lindi ni vituo muhimu vya biashara katika mikoa ya kusini mwa Tanzania. “Tunataraji kwamba wakazi wa Lindi na Mtwara, wafanyabiashara wanaojishughulisha na biashara ya korosho, uvuvi na wadau katika sekta ya mafuta na gesi watafurahia uzoefu wa teknolojia ya 4G LTE na kufanya shughuli za kijamii kwa njia ya mtandao kwa urahisi zaidi,”anafahamisha.

Anaongeza kusema, “Ninapenda kuwajulisha wateja wetu kwamba bei bei kwa ajili ya vifuurushi vya intaneti ya 4G LTE ni sawa na ile ya vifurushi vya 3G, na hali kadhalika wateja wote walio na kadi ya simu ya 4G LTE watanufaika kwa kupata GB 10 bure watakapojiunga kwa mara ya kwanza na mtandao wa 4G LTE. Hii inamaanisha kwamba mteja mwenye thamani anahitaji kuwa na kifaa kinachowezessha teknolojia ya 4G LTE, ama kiwa simu ya kisasa au kisambazio pamoja kadi ya simu. Wanaweza kubadilisha au kupata kadi ya simu ya 4G kutoka katika maduka yetu ya Lindi na Mtwara.”

Anaarifu kuwa mipango ipo njiani kupanua huduma hiyo hadi kufikia mikoa mitano iliyobakia na hivyo kuwa imesambazwa nchini kote ifikapo mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: