Pamoja na kuwa bora utoaji wa huduma za kibenki lakini pia benki ya NMB imejipanga kuhakikisha inakuwa pia bora katika kusaidia jamii na katika kudhihilisha hilo imetoa msaada wa vifaa vya kutumia darasani na vya michezo kwa watoto walio na usonji (autism) ambao wanasoma katika shule ya msingi Mbuyuni, iliyopo Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Akielezea kuhusu msaada huo, Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo alisema wameamua kutoa msaada kwa shule hiyo kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye usonji kusoma katika mazingira mazuri hasa kutokana na hali zao jinsi zilivyo.
Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya shuleni kwa wanafunzi wa usonji katika shule ya Msingi Mbuyuni.

"NMB kila mwaka tunatenga asilimia moja ya faida ambayo tunaipata katika kusaidia jamii, tumeshatoa misaada mingi kama madawati na sasa tuliona tuwasaidie watoto hawa na tunaamini msaada wetu utaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa," alisema Bi. Bishubo.

Kwa upande wa mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi aliwashukuru NMB kwa msaada ambao wamewapatia shule ya Mbuyuni na kuwataka kuendelea kuwa na moyo huo kwa kutoa msaada katika shule zingine zilizo na mahitaji.
Mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi akiwashukuru NMB kwa msaada ambao wamewapatia ambao unakadiriwa kuzidi Milioni 7.

Alisema licha ya serikali kufanya jitihada mbalimbali lakini bado inahitaji wadau wengine wa kusaidiana na kama kunakuwa na wadau kama NMB ambao wanajitoa kusaidia jamii basi wanakuwa wadau wa ukweli ambao wanaunga mkono juhudi za serikali kuleta maendeleo.

"Kwa nia yenu ya kusaidia jamii basi nyie mnaipatia kabisa serikali sababu inajitahidi kuleta elimu bora na hata kwa watoto hawa ambao bado kuna changamoto ya vifaa kwahiyo sisi tuwashukuru kwa msaada wenu na msisite tena kutusaidia siku tukiwafata kwa kuomba msaada," alisema Mushi.

Na Rabi Hume, MO BLOG
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbuyuni, Dorothy Malecela akitoa neno la shukrani kwani niaba ya uongozi wa shule na wanafunzi. (Picha zote na Rabi Hume - MO BLOG)
Mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi akimshukuru Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo kwa msaada ambao wamewapatia.
Mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi na Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo wakicheza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni.
Mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo ambavyo vitatumiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni.
Mwonekano wa baadhi ya vifaa vya michezo ambavyo NMB imetoa msaada kwa Shule ya Msingi Mbuyuni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: