Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba Haji Manara akizungumza na Waandishi wa habari leo kuunga mkono juhudi za Raisi John Magufuli za kuhamia Dodoma na kuridhia timu yake kwenda kucheza mechi ya kirafiki na Polisi Dodoma, Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoani Dodoma (DOREFA) Mulamu Nghambi.
---
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KLABU ya Simba imekubali mwaliko wa kwenda kucheza mechi ya kirafiki na Timu ya Polisi Dodoma ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Raisi Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli za kuhamia Mkoani Dodoma.

Mwaliko huo umeletwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma. Mwenyekiti wa Mulamu Nghambi amesema kuwa wao kwa pamoja wanaunga mkono juhudi za Raisi za kuhamishia makao makuu ya nchi mkoani kwao kwani zitaleta maendeleo makubwa.

Nghambi amesema, walituma maombi yao kwa uongozi wa klabu ya Simba na waKaonesha nia ya kushirikiana katika harakati hizo kwani mkoa wa Dodoma una mashabiki wengi wa timu ya Simba na mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba 03 kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wa Simba Haji Manara amesema kuwa wamefurahi kupata mwaliko huo na kwa kuwa hakuna ratiba ya ligi wikiend hii nawaahidi mashabiki wa Simba mkoani Dodoma kusubiri ujio wetu kwa shangwe zote.

"Katika kuhakikisha tunaunga hoja za Raisi John Pombe Magufuli za kuhamishia makao makuu ya nchi Mkoani Dodoma  na Chama cha Mpira wa Miguu mkoani humo kutupatia mwaliko tumeupokea kwa mikono miwili na tunawataka wanachama na mashabiki wa timu ya Simba kuja kushuhudia mchezo wetu na Polisi Dodoma siku ya Jumamosi Septemba tatu mwaka huu,"amesema Manara.

Kikosi cha Simba kitaondoka Alhamisi wakiwa na wachezaji wao wote waliosalia baada ya wengine kuwepo kwenye majukumu ya timu zao za Taifa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: