Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma akiongea na waandishi wa habari.

Na Woinde Shizza, Arusha.

Chama cha waandishi wa habari za michezo na Burudanimkoa wa Arusha (TASWA ARUSHA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Arusha Media wameandaa tamasha la 11 la waandishi wa habari za michezo na burudani kanda ya Kaskazini ambalo litafanyika Septemba 11 katika uwanja wa Generat Tyre.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma alisema zaidi ya watu 2500 wanatarajiwa kushiriki Tamasha hilo, ambapo kutakuwa na michezo ya Soka, Kuvuta kamba, Mbio za magunia ,Kukimbiza kuku na muziki kuanzia saa nne asubuhi hadi jioni.

Juma alizitaja timu ambazo zitashiriki ni TASWA FC kutoka jijini Dar es Salaam, timu ya Radio ORS kutoka mkoa wa Manyara, timu ya Sunrise Radio, Timu ya chuo cha uandishi habari Arusha, timu ya MJ Radio na timu ya Triple a Radio.

Katika tamasha hilo, pia kutakuwa na timu za vyuo vya uandishi habari vya mkoa wa Arusha, chuo cha habari Maalum, Tasisi ya habari na mawasiliano iliyopo maji ya chai, TASWA Arusha.

“Tamasha litatanguliwa na semina ya siku moja ya wanahabari mkoani Arusha juu ya masuala ya michezo, Utalii wa ndani na umuhimu wa Uwekezaji katika taifa”alisema

Mratibu wa Tamasha hilo, Andrea Ngobole alifafanua kuwa pia kuna timu ambazo zimealikwa ambazo ni Kitambi Noma, Timu ya TANAPA,timu ya TBL Arusha, timu ya PEPSI na Coca Cola na Wenyeji timu ya Wazee Klabu.

Ngobole alisema Septemba 3, TASWA na Arusha Media watatangaza zawadi kwa washindi, wadhamini wote na Mgeni rasmi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: