Warembo hao wakiwa mbele ya ghala zinamo hifadhiwa bia za Windhoek wakati wa ziara hiyo.
Mshauri wa Miss Kinondoni, Boy George (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya shindano hilo. Kutoka kulia ni Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabibo,Constantine Mwafulilwa, Andrea Missana, Mratibu wa Shindani la Miss Kinondoni Rhamat George na Mwalimu wa warembo hao, Neema Chaky.
Mratibu wa shindano hilo, Rhamat George (katikati), akizungumza katika mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale.
Mwanamuziki nguri wa muziki wa dansi hapa nchini Cristian Bella anatarajiwa kuwasha moto katika shindano la kumsaka Malkia wa Ulimbwende
Kanda ya Kinondoni linatarajiwa kufanyika kesho kutwa Ijumaaya katika Ukumbi wa Denfrances Sinza jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuwa kutanisha warembo hao na wadhamini washindano hilo ambao ni Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd ambao ni wasambaji wa kinywaji cha Windhoek Dar es Salaam jana, Ofisa Mauzo wa kampuni hiyo, Andrea Misama alisema maandalizi ya shindano hilo yanaendalea vizuri ambapo aliwashukuru warembo wote waliojitokeza kwenye shindano hilo kwa mwaka huu na kuwa mwanamuziki huyo akishirikiana na kundi la sanaa la kampuni hiyo watapamba jukwaa kwa kutoa burudani la kukata na shoka.
"Mwaka huu washiriki waliojitokeza ni wengi ukulinganisha na mwaka jana, hivyo tunatoa pongezi kwa wazazi waliowaruhusu watoto wao kushiriki, malengo yetu ni kukuza vipaji na kutoa ajira kwa wasichana ili waweze kutimiza ndoto zao”, alisema.
Kwa pande wao warembo watakaoshiriki shindano hilo wameahidi kuonyesha vipaji walivyonavyo na kuwaomba wadau na mashabiki waurembo kujitokeza kwa wingi siku ya shindano ili wawezekusapoti Miss Kinondoni.
Shindano hilo linashirikisha warembo 20 kutoka vitongoji mbalimbali vya Kanda ya Kinondoni ambapo kiingilio kitakuwa sh 10,000 na 20,000 kwa VIP huku shindano hilo likipambwa kwa burudani kutoka kwa mkali wa masauti Christian Bella.
Toa Maoni Yako:
0 comments: