Warembo walioingia tano bora wakiwa jukwaani
Kamati ya Miss Tanzania nao walikuwepo wakifuatilia shindano hilo ambalo lilifanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort mjini Tanga.
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akizungu mza wakati wa shindano hilo.
Msanii Nevy Kenzo akitumbuiza wakati wa shindano la kumtafuta mlimbwende wa mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016)lililofanyika hivi karibuni kwenye hotel ya Tanga Beach Resort
WAKATI shindano la kumsaka malkia wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016)likifanyika mwishoni mwa wiki na hatimaye mrembo Eligiva Mwasha kuibuka na ushindi kwenye kinyang’anyiro hicho dhidi ya washiriki wengine 10.
Shindano hilo ambalo lilisimama kwa muda baada ya serikali kulisimamisha lile la Taifa msimu huu lilionekana kuwa na msisimuko wa hali ya juu kuanzia wapenzi,wadau na washiriki iliyochangiwa na waratibu wa shindano hilo Radio ya Tanga Kunani FM (TK) wakishirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort.
Ushindani wa washiriki hao ulianza kuonekana tokea wakati warembo hao wakiwa kwenye kambi yao ambayo ilifanyika kwenye hotel hiyo ambapo kila mmoja alionekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kuondoka na taji hilo.
Hali iliendelea kuwa ya mvutano zaidi baada ya baadhi ya washiriki kuaga mashindano hayo na kutoa fursa yaw engine kuingia nafasi ya tano bora katika kinyanganyiro hicho ambacho kilihudhuriwa na wapenzi wengi kuliko kawaida.
Kitendo hicho kinaonekana kinawezesha kurudisha hamasa na heshima ya shindano hilo ambalo hufanyika kila mwaka mkoani hapa lakini pia kuhamasisha hasa vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki msimu ujao.
Katika shindano hilo nafasi ya pili ilichukuliwa na Aisha Ally huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Rukaiya Hassani katika shindano hilo ambalo lilikuwa na ushindani mkubwa kutokana na kusheheni warembo wakali.
Halikadhalika nafasi ya mrembo kwenye kipaji katika shindano hilo ilinyakuliwa na Edna Chisabo ambapo kinyang’anyiro hicho kilifanyika siku moja kabla ya onyesho la kumsaka mrembo wa mkoa huu kwenye ukumbi wa Tanga City Lounge uliopo mjini hapa.
Akizungumza mara kabla ya kutangaza mshindi wa Taji la Miss Tanga 2016, Mbunge Mussa alisema tasnia ya urembo imekuwa ikiwapa vijana maisha mazuri lakini pia imekuwa ni daraja la wao kupata mafanikio
Alisema lazima watanzania ikiwemo wazazi kubadilika na kuondokana na dhana ya kuwa ya kuwa urembo ni suala la uhuni kwani imekuwa ikisaidia vijana wengi kupata maendeleo.
"Ndugu zangu lazima tubadilike na kuishi kutokana na utandawazi uliopo ile dhana ya kuwa urembo ni uhuni mimi nadhani imepitwa na wakati na uhuni mtu anaweza kuwa nao hata asiposhiriki mashindano hayo hivyo wazazi na walezi ruhusuni watoto wenu washiri kwenye mashindano haya "Alisema.
"Neno la Mshindi wa taji la Miss Tanga 2016 Eligiva Mwasha" Alisema kuwa kwanza anawashukuru wakazi wa Mkoa wa Tanga kwa ujumla kwa sapoti yao walionyesha katika fainali za miss tanga 2016 na yeye kupata fursa ya kunyakua taji hilo
Licha ya kuibuka na ushindi lakini niwaombe niombea kwani kwa sasa safari aliokua nayo bado kubwa sana kwani anamtihani wakwenda kuiwakilisha Tanga katika fainali za Miss Kanda na badae kulekea Katika fainali za miss Tanzania baadae mwaka huu.


Toa Maoni Yako:
0 comments: