BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Jana tarehe 27/7/2016 limetoa uamuzi wa kuwafukuza kazi Watumishi 4 wa idara ya fedha baada ya kuthibitika wana utoro kazini na rushwa.
Aidha baraza hilo la madiwani limewashusha vyeo na madaraja wahandisi 2 kati ya 9 wa idara ya uhandisi huku 1 akishushwa daraja na onyo na 6 kuthibitika kuwa hawana hatia.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Jana, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob amesema hatua hizo zimechukuliwa baada ya kufanyika mkutano maalum wa mashauri na nidhamu uliofanyika jana na kuwajadili watumishi 18 waliofunguliwa mashauri.
Meya Jacob amesema uamuzi huo wa kuwapa onyo na kuwashusha madaraja na vyeo watumishi wa uhandisi umetokana na kushindwa kutumia taaluma yao vizuri kuishauri halmashauri namna nzuri ya maamuzi ya mabadiliko ya ujenzi wa barabara za biafra, journalism na barabara ya maandazi.
Wahandisi 2 waliochukuliwa hatua ya kushushwa vyeo na madaraja ni mhandisi mkuu Baraka Mkuya na mwenzake Ismail Mohamed huku mhandisi Daud Sigala akipewa onyo kali na kushushwa daraja.
"Baraza la madiwani limezingatia taratibu zote katakana kuchukua hatua za kibosh amusing dhidi ya watumishi hao ikiwa ni pamoja na kufanyika uchunguzi wa awali kuhusu tuhuma husika na kufungua mashtaka dhidi yao.
Watumishi kuwasilisaha ureter was ndani ya muda wa siku 14 baada ya kusimamishwa kazi na kuundiwa tume ya uchunguzi ambayo iliwasilisha taarifa kwa mammals ya nidhamu iliyotuwezesha kufikia maamuzi haya" abaseme Meya Jacob
Pamoja na hayo mkutano huo wa mashauri ya nidhamu ulijadili na kuridhia kutoa kibali cha kuwapandisha vyeo watumishi 372, kuwabadilisha vyeo watumishi 9 na kuwathibitisha kazini watumishi 206 ambao wamemaliza vipindi vya majaribio.
Toa Maoni Yako:
0 comments: