Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humudi Abdulhussein (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kimtandao na Bidhaa wa First National Bank, Silvest Arumasi (kulia) kwa niaba ya washindi kumi wa kampeni inayoendeshwa na benki hiyo kuhamasisha uwekaji akiba ili kujikwamua kiuchumi. Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es salaam leo. (Picha: Mpiga Picha Wetu).
Meneja Masoko wa First National Bank, Blandina Mwachang’a akiwapigia simu washindi wa droo ya kampeni inayoendeshwa na benki hiyo kuhamasisha uwekaji akiba ili kujikwamua kiuchumi ambapo washindi kumi walijipatia shilingi milioni moja kila mtu. Wengine kwenye picha ni Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humudi Abdulhussein (kushoto), Mtaalamu wa Mfumo wa Habari na Mawasiliano wa FNB, Bi. Ilakiza Hezwa (wa pili kushoto) na Meneja wa Sheria wa benki hiyo, David Sarakikya (kulia)
---
*Yatangaza washindi kumi wa kampeni ya Mama
First National Bank Tanzania imeendelea kuwahimiza Watanzania kujiwekea akiba benki ili waweze kujiinua kiuchumi na kujikwamua wakati wa dharula. Benki hiyo imetangaza washindi wa kwanza wa kampeni yake mpya ya kuhamasisha uwekaji akiba ijulikanayo kama kampeni ya Mama ambapo jumla ya washindi kumi wamezawadiwa shilingi milioni moja kila mtu kwenye droo iliyofanyika jijini Dar es salaam leo.
Akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi hizo leo, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kimtandao na Bidhaa wa FNB, Silvest Arumasi amesema jumla ya washindi 30 watapatikana kupitia kampeni hiyo itakayofanyika kwa miezi mitatu ikiwa na dhumuni la kuwahamasisha Watanzania kujiwekea akiba benki ili iwasaidie wakati wa dharula au kufanya shughuli za kujiinua kiuchumi.
Arumasi aliwataja washindi hao kuwa ni, Husna Hussein wa Mwanza, Pius Gobolo wa Dar es salaam, Prudence Kamanzi wa Dar es salaam, Tuddy Lutengano wa Dar es salaam, Wasonga Killion wa Mwanza, Ryoba Mwita wa Dar es salaam, Agnes Kihwele wa Mwanza, Joyce Kapya wa Dar es salaam, Suzzane James wa Mwanza na Violet Mordichai wa Dar es salaam.
“Inatia moyo sana kuona idadi kubwa ya Watanzania wanashiriki katika kampeni hii na tunaamini kwamba itasaidia sana katika kujenga utamadauni wa kuweka akiba ambao tunajitahidi kuujenga na kuuendeleza miongoni mwa Watanzania na vile vile tumefurahi kuona wateja wetu wakifanikiwa kujishindia zawadi kupitia kampeni hii”
Arumasi alisema kuwa dhumuni jingine la First National Bank kuanzisha kampeini hiyo ni kuwatunuku wateja wa benki hiyo pamoja na wateja wapya ambapo wateja uingizwa moja kwa moja kwenye droo kutokana na kila shilingi elfu hamsini wanayoweka kwenye akaunti zao za akiba.
Toa Maoni Yako:
0 comments: