Ilikuwa ni fainali mbovu kumalizia michuano mikali ya Euro 2016. Yaani Ureno, ambayo imenyakua ubingwa huo kwa goli moja la mshambuliaji wa zamani wa Swansea ya Uingereza Ederzito ‘Eder’ Antonio Macedo Lopes, timu iliyomaliza ya tatu kwenye hatua za makundi wamenyakua kombe wakiwa wameshinda mchezommoja tu kati ya saba ndani ya dakika 90. Hata hivyo Ureno inastahili sifa, kwanipamoja na kumpoteza nahodha wao na mchezaji Bora Cristiano Ronaldo alipoumia goti katika kipindi cha kwanza kwa kuchezewa vibaya na Dimitri Payet wa West Ham.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Ureno wakishangia kwa pamoja ushindi walioupata kupitia kwa Mshambuliaji, Ederzito ‘Eder’ Antonio Macedo Lopes (9) wakati wa mchezo wa fainali dhidi ya wenyeji wa Mashindano hayo, Ufaransa, uliochekwa katika uwanja wa Stade de France.
Eder dakika ya 109 aliwapachikia bao la kuongoza Portugal na kufanya 1-0 dhidi ya Wenyeji Ufaransa.Dakika 105 za dakika 120 zilikamilika nazo wakiwa bado 0-0Hadi dakika 90 zinakamilika Wenyeji France 0-0 Portugal na kuongezwa dakika 30. Wakati wa mapumziko kidogo baada ya dakika 90 kumalizika Cristiano Ronaldo alirudi kuwapongeza Vijana wenzake Portugal na kuwapa neno kuendelea vyema mpaka mwisho.Kipindi cha kwanza dakika ya 24 Cristiano Ronaldo aliumia na kulazimika kutolewa Nje ya Uwanja na kuifanya Portugal kuongozwa na Nani Nahodha.
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ureno, Christiano Ronald pamoja na Mkongwe Ricardo Quaresma wakiwa na mwali wao mara baada ya kutwaa kwa kuwagaragaza wenyeji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro 2016) katika mchezo uliopigwa katika dimba la Stade de France, nchini Ufaransa.
Huzuni baada ya kufungwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: