Mwalimu wa Karate wa kimataifa Sensei Rumadha 
 Magwiji wa karate duniani wakiwa katika picha ya pamoja katika kongamano la Karate European Jundokan Gasshuku.
---
Sensei Rumadha Fundi mwalimu wa karate mtanzania anatambuliwa na baraza  la OKINAWA  BODOKAN & KARATE FEDERATION" lenya makao Okinawa,Japan,juzi katika  alikuwa ni mwakilishi pekee kutoka Afrika katika kongamano la walimu  magwiji wa karate lilifanyika Lisabon, Ureno.

Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu ni chimbuko la dojo iliyo  jengwa na Master Eiichi Miyazato miaka 63 iliyo pita huko mjini Naha,  Okinawa baada ya kifo cha mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu ,  Master Chijun Miyagi , ambayo hivi sasa inaendeshwa na mtoto wake Yoshihiro Kancho Miyazato.


Sensei Rumadha Fundi, amepokea na kukubali mwaliko kama  mwakilishi wa "JUNDOKAN SO HONBU" Tanzania ikiwa natumaini la usajiri wa chama hicho hapa Tanzania ambao kwa sasa bado unalegalega.

Sensei Rumadha yupo nchi Ureno hivi sasa akishiriki katika kongamano la Karate " European Jundokan Gasshuku 2016".

Na wakati huohuo, kitengo kinachisimamia ubora na uthabiti wa  sanaa asili ya mitindo ya karate toka Okinawa kiitwacho " OKINAWA  BODOKAN & KARATE FEDERATION" imefanya mabadiliko hivi karibuni  yatakayo tofautisha karate asilia na ile ya kimichezo itayo kuwa  katika michezo ya Olympics.


Kutokana na mabadiliko ya kimbinu na ufasaha yanayo onekana  katika michezo, shirikisho hilo limeamua kutofautisha kabisa jinsi  karate asilia izidi kuimarika na kutochujwa na kuwa sanaa nyepesi.

Pia, kuhakikisha kwa kiundani zaidi kwamba mbinu halisi, zinazingatiwa na ma- Sensei wote wa mitindo ya karate toka visiwani Okinawa duniania kote.

Hivyo ime teuwa timu ya Karate ya Okinawa ( Masters) toka mitindo mbalimbali inayo tambulika na " BUDOKAN" kusambaza uadilifu wa mitindo hiyo kama jinsi ilivyokuwa inafundisha na waasisi wake asilia.

Semina hii inayoendelea nchini Ureno inawawezesha walimu (Sensei) kuwa na mabadiliko au kuendana sambamba na jinsi sanaa inavyo jadiliwa katika chimbuko lake chini ya shirikisho hilo huko Okinawa, Japan.

Tunatumaini kwamba chama cha "JUNDOKAN SO HONBU" kitapata usajili wake nchini Tanzania pasipo fika mwaka 2018, chini ya Sensei Rumadha Fundi mwakilishi wa "JUNDOKAN SO HONBU" Afrika mashariki na Kati. Endapo usajili utaleta kulegalega na kuvuta muda zaidi, basi chama hicho hakitakuwa na budi, bali kitajisajili visiwa vya Zanzibar kwanza. Alimalizia hivyo; sensei Rumadha
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: