Wawakilishi toka Serikali za mitaa, Serikali ya mkoa na Serikali kuu, sekta binafsi na taasisi za kijamii za kiraia zinakutana leo tarehe 20 Juni mjini Arusha ikiwa ni mkutano wa tatu wa wadau wa mpango mji wa Arusha 2035.

Timu yenye wataalamu kutoka jiji la Arusha,Mkuu wa wilaya wa Arusha na Meru Arusha, tume ya undeshaji ya Mkoa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi watazindua Rasimu ya Mwisho ya Mpango Mji Kabambe wa Arusha 2035 , wakisaidiwa na mshauri mtaalam aliyeteuliwa toka Singapore, Surbana International Consultants

Maeneo ndani ya mpango mji itachukua kilometa za mraba 278 za mji wa Arusha na kilometa za mraba 330 zilizochaguliwa za wilaya ya Arusha na Arumeru zikifanya jumla ya kilometa za mraba 608.

Rasimu hii ya Mwisho ya mchoro pendekezi itaonyesha matumizi ya siku zijazo ya ardhi ndani ya eneo linalopangwa . Pamoja na haya utaonyesha mpango mzima wa usafirishaji na barabara, mpango wa aina mbali mbali za barabara, miundombinu na usafirishaji wa mizigo utaelezwa kwa kina.

Hali kadhalika mchoro pendekezi unaoonyesha mpango mzima wa miundombinu utaelezewa kwa kina, hii ni pamoja na mpango kazi na mtandao wa maji safi na maji taka, maji ya mvua, taka ngumu, mfumo wa umeme na mtandao wa mawasiliano ya teknolojia. Maendeleo ya uchumi wa pamoja na ulinzi wa mazingira itakuwa ni sehemu kubwa ya mada. Michoro ya usanifu wa kina utawasilishwa kuonyesha uwezo wa kijamii na kiuchumi wa siku zijazo “Mji Mkuu Kijani wa Afrika Mashariki”.

Uwasilishwaji wa Rasimu na wataalamu utakamilishwa na maelezo ya kina ya “Mpango wa Utekelezaji”. Mpango pendekezi unalenga kuwa wa maono lakini pia uoneshe uhalisia kwa hivyo umuhimu wa uundaji wa hati maalum yakusaidia utelekelezaji wa mpango huu.


“Rasimu ya mwisho ya michoro ni hatua muhimu kwa mkoa wetu. Mahitaji ya baadaye kwa ajili ya mji wetu unaokua, unatuhitaji kuwa na mipango ya nyumba zaidi, miundombinu bora, mipango ya maendeleo bora kwa ajili ya viwanda, makazi na maeneo ya kijani kwa njia inayojali mazingira. Hii rasimu ya mwisho inatupa fursa ya kuweza kutengeneza mji wa kijani, kitovu cha kanda, na kuonyesha mfano wa ufanisi katika upangaji wa mji” alisema Juma Idd Mkurugenzi wa Jiji la Arusha.

Mkutano wa kwanza wa wadau ulifanyika Mei mwaka 2015, ulizungumzia mchanganuo wa muktadha wa kanda kwa wadau na pia kupendekeza mtazamo na mpangilio wa siku zijazo wa mamlaka ya jiji la Arusha. Mtazamo wa jumla wa matokeo ya waatalaam ya mkutano wa wadau uliopita utajadiliwa mbele ya wadau watakaokuwepo.

Huu ilifuatiwa na mkutano wa pili wa wadau Novemba 2015, na mkutano wa wataalam Dar es Salaam , Disemba 2015.

Lengo la mkutano huu wa mwisho wa wadau kama ilivyoagizwa na Sheria ya Mipango ya mwaka 2007 ni kuidhinisha hii Rasimu ya mwisho. Hatimaye Rasimu ya Mwisho ya Michoro itatumwa kwa madiwani, kwa Katibu Tawala wa Mkoa na kwa Mkurugenzi wa Mipango Miji kwenye Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Baada ya kuipitia, jamii itapata fursa ya kushiriki kikamilifu, kukusanya maoni na mapendekezo, kabla ya idhini ya mwisho kutoka kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Hatua hii shirikishi inalenga kupokea mchango muhimu wa kuboresha mpango mji wa Arusha kutoka kwa wadau wote.

Wananchi wote watajulishwa mara kwa mara kuhusu hatua za maendeleo za mpango mji kupitia vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni machapisho, na mitandao ya kijamii. Watu wote wanakaribishwa kutoa maoni yao juu ya mpango mji.

Kupitia Facebook: Arusha 2035, Instagram: Arusha2035 na Twitter: Arusha_2035, kwa kutoa maoni yao kwenye sanduku la maoni katika wilaya na ofisi za kata au baruapepe: arusha2035@gmail.com.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: