Vikao vya Bunge vimeendelea leo June 20 2016, huko Bungeni Dodoma ambapo wabunge wa Upande wa Upinzani wamekuwa na mfululizo wa kutoka Bungeni pale anapoongoza Bunge Naibu Spika Dk. Tulia Akson. Kali ya leo Juni 20, 2016 Wabunge wa Upinzani wameendelea kususia vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, huku wakitoka bungeni kwa mtindo mpya wa kuziba midomo na karatasi.
Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi) James Mbatia amesema wameanza kutoka kwa kufunga midomo na karatasi kuiambia dunia kuwa bajeti imejaa ghiriba na udanganyifu mwingi kwa Watanzania. Cha kujiuliza je hii ni dawa??????
Pichani ni wabunge hao wakiwa na vitambaa mdomoni.
Toa Maoni Yako:
0 comments: