Kamanda Mstaafu wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam akiagwa katika gari wakati wa sherehe rasmi iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Uaskari (MPA) zamani ilijuliakana kama CCP.
Leo June 22 aliyekuwa Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ameagwa rasmi kwenye viwanja vya Chuo cha mafunzo ya taaluma ya Uaskari Moshi (MPA).
 
Kamanda Kova alihamia Dar es Salaam mwaka 2008 akitokea mkoa wa Mbeya ambapo Disemba 31 2015 alistaafu rasmi kulitumikia Jeshi la Polisi Tanzania, mafanikio yanayosemwa na Kamanda Kova mwenyewe aliyoyafanya ni kupunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya kiuhalifu, yaliyokuwa yanaitikisa nchi hususani matukio ya wizi na uvamizi wa kwenye benki.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: