Mama mmoja alifukuzwa na mumewe kwa sababu alikuwa ametoka kujifungua mtoto wa kike na pia alikuwa tayari na watoto watano wote wa kike, jambo lililomuudhi yule mme wake kwani yeye alihitaji mtoto wa kiume.
Mme huyo alikuwa na utajiri mkubwa lakini akamwacha mkewe akihangaika na watoto hao sita bila hata ya msaada wa matunzo.
Mama ikambidi atumie muda wake kufanya kazi kwenye majumba na mashamba mbalimbali ili ya watu aweze kuwatunza wanae na kuwapa elimu bora.
Maisha yalikuwa magumu kwani alikosa nguo za kuvaa na kupewa msaada wa marafiki na majirani, kwa kweli maisha yalikuwa magumu kupindukia.
Leo hii wale watoto sita wote wamefanikiwa kuhitimu vyuo na wameajiriwa sehemu tofauti, mmoja ni daktati, mwingine ni mwalimu, mwingine ni mfamasia, mwanasheria, injinia na mwingine ni mfanyabiashara aliyeolewa na mme mwenye fedha nyingi sana.
Yule mama kwa sasa ameboreshewa ofisi yake na kupewa mtaji wa biashara kubwa na anazunguka kutoka mji mmoja kwenda mwingine kibiashara na kusalimia wanae huku akifurahia mafanikio ya wanae.Ukimwangalia mama hata mavazi yake ni ya kumpendeza na ya gharama tofauti na mwanzo.
Hivi sasa yule baba aliachana na mke wake aliyekaa nae kwa muda mchache kwani naye alizaa watoto wa kike na sasa baba hana kazi na maisha yamekuwa magumu kwani alitumia muda na fedha nyingi kuhangaikia kupata mtoto wa kiume.
Mama sasa anakaa na kufurahia matunda ya watoto wake na kasahau maumivu aliyoyapitia zaidi ya kumshukuru Mungu kwa kumpa afya njema yeye na wanae na kumshukuru pia kwa kuwa msaada wake mpaka amefanikiwa kuwakuza wanae.
Ndugu yangu, Mtoto ni mtoto awe wa kike au wa kiume.. ...
Jambo la msingi ni kumshukuru Mungu na kuomba ulinzi wake na kuhakikisha unajituma kuwaandalia maisha mazuri wanao kwani ni mafanikio yako ya kesho.
Jiwekeze kwa wanao na utakula matunda ya upendo wako uliowapa kutoka kwao, matunzo yako kwao yatarejea kwako mara dufu na hata furaha yako kwao na elimu uliyowapa vitakuwa hazina yako ya kesho na ulinzi.
Sala yangu rahisi kwako: Kila mtu aliyekukataa leo atashangaa hadithi ya maisha yako itakapo badilika kesho.
Naomba haya nikiamini Mungu anasikia sala zetu.
Amen.
Toa Maoni Yako:
0 comments: