Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea wakati wa ufunguzi wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars kwa viongozi wa mikoa iliyofanyika leo (Julai 7, 2015) jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti soka la vijana wa TFF Ayoub Nyenzi na Kushoto ni Mwenyekiti msaidizi soka la vijana wa TFF Khalid Abdallah.
 Mkurugenzi wa ufundi wa TFF Salim Madadi akiongea wakati wa wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars kwa viongozi wa mikoa iliyofanyika leo (Julai 7, 2015) jijini Dar es Salaam. Katikati Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akifatiwa na Mwenyekiti soka la vijana wa TFF Ayoub Nyenzi
 Mwenyekiti soka la vijana wa TFF Ayoub Nyenzi akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa Semina elekezi ya michuano ya Airtel Rising Stars iliyoshirikisha wasimamizi na viongozi wa mikoa itakayoshiriki katika michuano ya Airtel Rsing Stars inayotegemea kutimua vumbi 20 Julai. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando na kulia ni baadhi ya viongozi wa TFF
Viongozi soka kutoka katika mikoa inayoshiriki michuano ya Airtel wakifatilia Seminar elekezi ya Michuano ya Airtel Rising Stars iliyofanyika iliyofanyika leo (Julai 7, 2015) jijini Dar es Salaam. Mikoa inayoshiriki katika michuano ya mwaka huu ni pamoja na ya Mwanza, Morogoro, Mbeya, Temeke, Ilala and Morogoro kwa upande wa wasichana huku mikoa ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Mbeya, Mwanza and Arusha ikiwa ni kwa upande wa wasichana
---
Shirikisho la Soka nchini (TFF), limewasisitiza viongozi wa soka ngazi za mikoa kutambua kuwa lengo kuu la michuano ya Airtel Rising chini ya vijana wa miaka 17, ni kuibua vijana kwa manufaa ya Taifa kwa baadaye na sio kulelekeza nguvu zao katika kupata matokeo mazuri uwanjani kama ambavyo watu wengi hufikiri.

“Tumegundua kwamba baadhi ya viongozi wa soka mikoani wana fikra tofauti na lengo la michuano hii, wao huangalia zaidi kupata matokeo mazuri uwanjani kuliko kutafuta vijana wenye vipaji kama lilivyo lengo la michuano hii. Na hii ndio sababu kuu ya ongezeko la tatizo la watu kuleta vijana waliozidi umri uliolengwa katika program hii”, amesema

Mwesigwa amemimina pongezi kwa kampuni ya Airtel nchini kwa kuamua kuwekeza katika soka hapa nchini hasa la vijana. “ Michuano ya Airtel Rising Stars imekuwa ni chachu kubwa hasa kwa upande wa soka la wanawake, ambapo idadi kubwa ya wachezaji wanatokana na progamu hii”, amesema Mwesigwa

Ameongeza kuwa soka la vijana limekuwa ni njia ya uhakika na endelevu katika maendeleo ya soka hapa nchini. “Kwa mfano nchi ya Cameroon, wamepata mafanikio makubwa na ya kuvutia kutokana na kuwekeza katika program za vijana”, alisema, huku akiiongeza pia Hisapania kama nchini nyingine ambayo ilifanya hivyo na kufanikiwa kuchukua kombe la dunia. Mwesigwa amewataka viongozi wa soka ngazi mbalimbali nchini kufuata taratibu na kanuni za michuano hii. “Nataka muelewe kuwa hii ni program muhimu na nyeti sana kwa taifa, kwa sababu inalenga hasa
vijana ambao wanahitaji uangalizi wa karibu sana ili kutimiza ndoto zao.

Kama ukiwafundisha kuwatii waamuzi, basi watafanya hivyo katika kipindi chote cha maisha yao ya soka, na endapo ukiwafundisha kutowatii waamuzi basi pia watafanya vivyo hivyo,”alisema huku akiwaonya vikali viongozi kutowapandikiza wachezaji imani za kishirikina.

Michuano hiyo imepanga kuanza kutimua vumbi katika ngazi ya awali (mikoa) julai 20 na kuhitimishwa Agusti 30, ambapo ngazi ya taifa itaanza Septemba 11 hadi 21 jijini Dar es Salaam. 

Kwa upande wake, Meneja Mahusiano wa Aitel nchini Jackson Mmbando amesema kuwa hii ni fursa nyingine tena adhimu kwa vijana kuonesha vipaji vyao ambavyo vitawawezesha kutimiza malengo yao ya baadaye kupitia mchezo wa soka.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: