Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris, (Kulia) akimpa
mkono na Bw. Festo Sakaya (kushoto) baada ya mteja huyo kujinunulia
friji la kisasa ndani ya banda lao la maonyesho ya Sabasaba ambapo baada
ya kufanya manunuzi alizawadiwa microwave ya bure, ya LG. Kampuni hiyo
ipo kwenye promosheni ya punguzo la bidhaa zake kwa asilimia 15 kwa
msimu huu wa sabasaba na ramadhani. Katikati ni meneja wa tawi la LG
Mtaa wa Nkurumah Bw. Yasin Lodhi.
Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris, (Kushoto)
akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya microwave ambayo inatolewa kama
zawadi kwa wateja wanaonunua friji za kisasa za LG. Tukio hilo
lilifanyika katika banda la LG ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya
biashara kimataifa maarufu kama Sabasaba, wa pili kushoto ni meneja wa
tawi la LG Mtaa wa Nkurumah ,Yasin Lodhi.
Bw. Festo Sakaya akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupokea
zawadi ya Microwave ya kisasa toka LG ambayo aliipata baada ya kufanya
manunuzi ya friji la kisasa ndani ya banda la LG wakati wa maonyesho ya
39 ya biashara kimataifa maarufu kama Sabasaba.
Meneja wa tawi la LG Mtaa wa Nkurumah, Yasin Lodhi, (kulia) akikabidhi
zawadi ya Microwave kwa Bi. Hidaya Kapera, (kushoto) mara baada ya mteja
huyo kufanya manunuzi ya bidhaa za kisasa ndani ya banda la LG katika
maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba.
Hidaya Kapera, akiondoka na zawadi yake ya Microwave baada ya kufanya manunuzi ya bidhaa za kisasa ndani ya banda la LG katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba.


Toa Maoni Yako:
0 comments: