Mohammed Iqbal Hajji, Mkurugenzi wa Azimio Estate Limited akiongea wakati na waandishi wakati wa Ziara wa Waziri Christopher Chiza, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji aliye tembelea mradi wa Dege Eco Village project ilio Kigamboni. (kushoto Waziri Christopher Chiza na Mkurugenzi wa miradi NSSF Bw Msenembo).
Mhe. Christopher Chiza akipokelewa na waandisi ambao ndiyo wajenzi wa mradi huu wa Dege Eco Village. Pamoja na Waziri ni Mkurugenzi wa Azimio Estate Limited na wageni wengine.
Adam Jusab, Meneja wa Masoko wa Dege Eco Village akiongea na wageni waliotembelea tukio hiloi lakuongea na wageni kuhusu mradi huo hivi jana hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Frank Isaack Chikoma, Meneja Mauzo wa Dege Eco Village akiongea na wageni waliotembelea tukio hilo lakuongea na wageni kuhusu mradi huo hivi jana hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu.
WAZIRI wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Christopher Chiza, amesema kuwa Mradi wa ujenzi wa nyumba wa Dege Eco Village, utasaidia kupunguza mlundikano wa watu Dar es Salaam.
Alisema kuwa wamiliki wa mradi huo, wanatakiwa kujenga nyumba zenye ubora mikoani kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma bora ya nyumba kwa jamii.
Waziri huyo aliyasema hayo wakati alipotembelea mradi huo ambao umeanza kujenga nyumba katika eneo la Kigamboni kwa ajili ya makazi ya watu.
Alisema kuwa kama Dege watafanikiwa kujenga nyumba kama hizo mikoani, zitasaidia kwa kiasi kikubwa mlundukano wa watu Dar es Salaam kwani hwatakuwa na haja ya kuja tena kutokana na kupata nyumba zenye ubora na kwa bei nafuu.
Alisema kuwa mradi huo ulianza mwaka jana ambapo unatarajiwa kumalizika mwaka 2017, na watu mbalimbali watapata fursa ya kununua nyumba hizo.
"Mradi huu utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza mlundikano wa watu Mkoa wa Dar es Salaam, kama nyumba zingine zitajenga mikoani, kwani watu wengi hawatakuwa na sababu za msingi za kuja kujenga Dar es Salaam," alisema.
Naye Mkurugenzi wa Mradi wa Dege, Muhammad Ikbar, alisema kuwa mradi huo unatarajiwa kujenga zaidi ya nyumba 700 kwa ajili ya watu mbalimbali.
Alisema kuwa baadhi ya nyumba zimeshawekewa oda mpaka sasa ambapo, wanajenga majengo ya kisasa ambapo watu watakaoishi ndani ya kijiji hicho hawatakuwa na sababu ya kwenda kutafuta mahutaji sehemu nyingine.
"Mradi huu umeanza mwaka jana, ambapo unatarajiwa kukamilika mwaka 2017, tunajenga nyumba zaidi ya 700 ambapo mahitaji yote muhimu yatakuwa yakipatikana ndani ya kijiji," alisema.


Toa Maoni Yako:
0 comments: