Dk Slaa na mkewe Josephine na Meya wa Indianapolis.
Dk Slaa akitoa muhadhara.
Dk Slaa, mkewe Josephine na wataalamu wa Katiba, Profesa  J.M Curtis na Dickson Ramsey.

Na Andrew Msechu.

KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa amesema Tanzania imedumaa kutokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimetawala kwa miaka zaidi ya 50 kushindwa kurutubisha rasilimali kwa manufaa ya wananchi na kwamba njia pekee ya kulikomboa taifa  ni kukiondoa madarakani
kupitia sanduku la kura.

Dk. Slaa alisema CCM ni sawa ni saratani inayolitafuna taifa, kutokana na serikali yake kukosa maadili na kukumbatia makundi ya wahalifu waziwazi bila hata kuona aibu, huku wananchi wake wakiendelea kuteseka na kwamba Watanzania wameendelea kuwa wabeba mizigo badala ya kuwa washindani katika uchumi wa dunia.

Akiwahutubia mamia ya wanazuoni katika Chuo Kikuu cha Purdue, nchini Marekani, Dk. Slaa alisema njia pekee ya kulinusuru taifa na saratani hiyo, ni kuleta mabadiliko ya kweli kupitia sanduku la kura na kwamba tiba ni kumpata rais atakayetokana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

“Bila shaka, haya ni mambo muhimu ambayo yanahitaji tuyazungumze sisi kama Watanzania  kwa kushirikiana na wadau wetu na marafiki kama nyie. 

Tunahitaji msaada wenu katika kukabiliana kuiondoa saratani hii CCM ili tuijenge jamii yetu kiuchumi,”alisema Dk. Slaa. Alisema.

Ziara ya Dk. Slaa nchini humo inatokana na mwaliko wa Gavana wa Jimbo la Indiana, Mike Pence pamoja na taasisi mbalimbali za nchini humo vikiwamo vyuo vikuu kutokana na kutambua mchango wake wa kisiasa na kijamii na chama chake katika maendeleo ya Bara la Afrika.

 Mbali na Chuo Kikuu cha Purdue, pia Dk. Slaa anatarajiwa kutoa mihadhara katika vyuo vikuu vya Indiana na Marion.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: