Watu kadhaa wamepoteza maisha baada ya basi la abiria la Nganga linalofanya safari zake kati ya Iringa na Kilombero lilipogongana kugongana uso kwa  uso na lori aina ya Fuso na kisha magari hayo kuteketea kwa moto  maeneo ya Milimani kilomita  kadhaa kutoka Ruaha Mbuyuni kuelekea Morogoro, majira ya asubuhi ya leo. Pichani ni basi hilo la Nganga wakati na bada ya kuteketea kwa moto. Endelea kuunana nasi tutawaletea habari kamili.

Eneo la ajali ni iyovi lililopo safu ya Milima ya Uduzungwa kando ya Mto Ruaha Tarehe 12/04/2015 majira ya Saa mbili asubuhi bus T.373 BAH Kampuni ya Nganga Express lililokuwa linatokea Kilombero kwenda Mbeya likiwa kwenye mistari ya barabarani ya katazo likiwa kwenye milima huo likiwa kwenye mwendo kasi, gari hilo liligongana na Mistubishi Fuso T.164 BKG iliyokuwa imebeba matikiti kisha kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu 15 kutoka kwenye basi na 3 kutoka kwenye Fuso na majeruhi 10 ,wanawake 4 na wanaume 6 ,ambapo wanne wamelazwa Hospitali ya ST.Kizito Mikumi na Sita Hospitari ya Mtandika Iringa.

Aidha kwenye basi kulikuwa kuna pikipiki iliyoungua ambayo inawezekana ndio iliyosababisha moto kuwaka na kuunguza bus na fuso.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: