Mamia ya waombolezaji jana Septemba 23, 2014 walijitokeza kwa wingi kumuaga mpendwa wao Marehemu Bi. Stellah Sagala ambaye alifariki Septemba 20, 2014 jijini Dar es Salaam. Marehemu Stellah alikuwa ni mfanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ameacha Watoto watau na mume. Alizikwa katika makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Padre akibariki mwili wa marehemu Stellah Sagala kabla haujaingizwa kanisani.
Waombolezaji wakiingiza mwili kanisani.
Waombolezaji wakiuaga mwili wa marehemu Stellah Sagala.
Watoto wa marehemu wakiaga.
Mume wa marehemu akiaga.
Mwili wa marehemu ukifikishwa makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam.
Kaka wa marehemu akipiga picha za ukumbusho.
Mume wa marehemu akitupia udogo wa mwisho.
Watoto nao wakimuaga mama yao kwa kutupia udogo wa mwisho.
Familia.
Toa Maoni Yako:
0 comments: