Tukio hili limetokea eneo la Bonanza kata ya Chamwino, Dodoma mjini. Kwa shuhuda wetu aliyekuwa eneo la tukio amesema kuwa dereva wa bodaboda amekutwa amefariki baada ya kuuliwa na watu wasiojulikana na kisha watu hao kutoweka bodaboda aliyokuwa akiendesha marehemu huyo. Dereva huyo wa bodaboda amechomwa kisu maeneo ya tumboni na shingoni katika mwili wake na katika eneo la tukio kumekutwa visu viwili amavyo vinasadikika kutumiwa katika uharifu huo kando kidogo ya barabara na sehemu ulipokuwa mwili wa marehemu.(Picha na Alex wa Pamoja Blog)
Hiki ni mojawapo ya kisu kinachosadikiwaa kutumika katika kufanya mauaji hayo ya dereva wa Bodaboda na kisha watu hao kutoweka na pikipiki.
Damu ikiwa imetapakaa eneo la tukio
Hii ni mojawapo ya sehemu aliyochomwa kisu dereva huyo wa bodaboda
Baadhi ya mashuhuda wakiwa kwenye eneo la tukio
Toa Maoni Yako:
0 comments: