Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
KAMPENI kubwa ya kuhamasisha usafi iliyokuwa inaendeshwa kampuni ya Green Waste Pro Ltd katika kata tatu za katikati ya jiji imemalizika kwa ufanisi mkubwa kiasi cha kufanya eneo hilo kumeremeta tena.
Kampeni hiyo ambayo ilianza Septemba 6 mwaka huu ilifungwa kwa usafi katika kata ya Kivukoni ambapo kampuni ya TICS ilishiriki kufanya usafi katika fukwe za bahari.
Katika kampeni zilizoshirikishwa wadau mbalimbali wa mazingira na afya katika kuhamasisha usafi miongoni mwa wananchi pamoja na kufanya usafi viongozi walitumia nafasi hiyo kufunza watu umuhimu wa kushiriki katika kufanya usafi na kuwa wasafi.
Kata zilizohusika na kampeni hiyo ni kata ya Kisutu, Mchafukoge na Kivukoni.
Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa alisema usafi huo umelenga kuweka maeneo ya bandari kuwa masafi na japokuwa wao wapo Temeke waliona kuna kila sababu ya kushiriki usafi kwenye maeneo ya bahari ambayo wanafanyia kazi.
Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Bw. Renatus Ruhungu alisema kampeni hiyo ambayo imefanikiwa, ilikuwa inawakumbusha wananchi wajibu wa kushiriki katika kuweka maeneo safi .
Toa Maoni Yako:
0 comments: