Wajumbe wa Bunge maalumu la katiba wameendelea kujadili rasimu ya kanuni zitakazo waongoza katika mjadala wa kujadili rasimu ya pili ya mabadiliko ya katiba ambapo suala la upigaji wa kura limekuwa mjadala mkali kutoka kwa wajumbe waliopata nafasi ya kuchangia.

Baadhi ya wajumbe ambao ni viongozi wa serikali pamoja na wabunge wa chama cha Mapinduzi (CCM) wametaka upigaji wa kura ufanyike kwa uwazi wakati baadhi ya wajumbe ambao ni wabunge wa vyama vya upinzani pamoja baadhi ya makundi wakitaka suala la upigaji kura lifanyike kwa siri.

Akitoa mchango wake wa kanuni hizo Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu Mheshimiwa Steven Wassira amesema wajumbe wote ni jamii moja pamoja na kuwa na utofauti wa mawazo anapendekeza kura itakayopigwa iwe ya uwazi kwakuwa hata mataifa mengine yanapiga hivyo.

Kwa upande wake mjumbe mwingine Philemon Ndesamburo akitoa maoni yake kuhusu upigaji wa kura amesema kura ya siri ni muhimu sana kwani ndio njia itakayosaidia kuondoa tofauti katika mjadala huo hivyo suala la uwazi litumike katika kuhesabu kura zitakazopigwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: