Serikali imeahidi kuangalia uwezekano wa kuwafadhili wanafunzi wapatao 20 kutoka katika mikoa ya Lindi na Mtwara wanaosoma katika chuo kikuu kishiriki cha Stella Maris kilichopo mkoani Mtwara (STEMUCO) ambao hawana uwezo wa kulipa ada ya masomo yao.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi wakati akimjibu Mhadhiri wa Chuo hicho Padre Aidan Msafiri ambaye aliwasilisha mada yake ya Tunu na maadili katika rasilimali za gesi, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania siku ya pili ya kongamano la viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara.

Katibu Mkuu MASWI amesema kuwa serikali ipo tayari kuhakikisha inawapatia elimu hiyo ili waweze kuhudumia jamii ya wananchi wa Lindi pamoja na Mtwara katika kujiletea maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Bwana Yona Killagane amesema kuwa zipo faida nyingi za mradi wa gesi kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kujenga shule za chekechea, wanafunzi kupata udhamini wa kusomeshwa shule za sekondari, kujenga hospitali, maji safi, ajira na kupata umeme unaotokana na gesi katika maeneo yao.

Kongamano la viongozi wa dini ni mwendelezo wa kongamano lilofanyika mwezi januari mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo kauli mbiu katika makongamano hayo ni“Rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: