Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini, Bwana Lephy Gembe akiwasili katika kata ya Mpunguzi katika shughuli za uhamasishaji wa kutumia vyakula vyenye virutubushi ambao unafanywa na USAID kupitia mradi wake wa Tuboreshe Chakula.
Mkurugenzi Mkazi wa mradi wa Tuboreshe Chakula, Unaofadhiliwa na Shirika la misaada la watu wa marekani USAID Bi Rebecca Savoie katikati, akitoa paketi ya unga wa uji uliochanganywa na virutubishi kwa mmoja wa wakazi wa kata ya Mpunguzi aliyehudhuria uhamasishaji wa lishe kwenye kata hiyo.
Mkurugenzi Mkazi wa mradi wa Tuboreshe Chakula, Unaofadhiliwa na Shirika la misaada la watu wa marekani USAID Bi Rebecca Savoie katikati, na maofisa wenzake kutoka mradi huo wakifurahi na wananchi wa Mpunguzi kwa kupiga makofi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya lishe kwenye kata hiyo leo.
Mmoja wa wahamasishaji wa umuhimu na faida za virutubishi kwa watoto wenye umri wenye miezi 6 mpaka miaka 5,Tom David, akiwagawia uji uliopikwa ukaongezwa virutubishi,wamama wa kata ya mpunguzi,wenye watoto umri wa miezi 6-miaka 5.Ikiwa sehemu ya uhamasishaji na uelimishaji kwa vitendo.Kampeni hizi zinadhaminiwa na mradi wa USAID Tuboreshe chakula.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: