04/01/2013 - 05/01/2013
Rais wa IBF Africa Onesmo Ngowi katikati akionesha mzani waliopimia mabondia Thomasi Mashali kushoto na Fransic Cheka kulia katikati ni Promota wa mpambano huo Adamu Tanaka picha na mpambano wao utakaofanyika siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' akipimwa Afya leo kwa ajili ya mpambano wake
Bondia Amos Mwamakula akipimwa Afya
Baadhi ya mabondia watakaopambana kesho wakiwa katika picha ya poz wa pili kushoto ni Thomas Mashali, Shabani Mhamila 'Star Boy' Ibrahimu Class' King class Mawe' wengine ni wapambe wao katika mchezo huo.
 Judges – from left to right Ms . Judy McDonald, Mr. Ulric Charteris, Mr. Bongai Zamchiya, Ms. Sally Westwood, Ms. Rudo Myangulu, Mr. Oscar Habeenzu, Mr. Mudiwa Mundawarara.

Ulric Charteris, Executive Creative Director at Roots255 in Dar es Salaam, recently accepted the invitation to be the external Judge chairing Zimbabwe’s Ngoma Awards. The Awards ceremony is Zimbabwe’s grandest stage for recognising excellence in their advertising industry.

This was the first time any individual working in the Tanzanian advertising industry officiated at an advertising ceremony on the continent. “It was an honour to participate in judging work from my peers in another African country,” Charteris commented. Charteris enhanced the Ngoma Awards committee with his deep experience in the advertising industry, gained from being a creative director of South Africa’s largest advertising agency, FCB, and regional creative director for Ogilvy Africa. Charteris has a thorough understanding of African markets having worked in countries like Tanzania, Ghana, Botswana, Uganda and Mozambique. Despite Charteris’ vast international experience and success, his trip to Zimbabwe was a fresh experience for him. “I’d never actually been to Zimbabwe, so it was an opportunity I never would have missed. I have always had a keen interest in the Zimbabwean advertising scene, especially having seen the high standard of work by Zimbabwean creatives in Tanzania and at our affiliate office in Botswana. I was very impressed and inspired by the creative work at the Ngomas,” concluded Charteris.
Ulric Charteris (Executive Creative Director Roots255 ) Praxie Dzangiare (Chariperson ZAPA)

Charteris also held workshops with the top creatives and agency owners in Zimbabwe on how to improve the quality of Afro-centric work in their country and on the continent as a whole. “Zimbabwe has many of the same challenges as we do in Tanzania,” said Charteris. “But sharing our experiences and collaborating to find common solutions is a step forward to creating our own, African voice in communications.”

Internationally Charteris is has also garnered top industry awards, including Cannes Lions in France, Clios (for five years consecutively) and the One Show awards in the United States. Meanwhile in the South African market he has also won two Grand Prix and a host of Gold, Silver and Bronze awards in South Africa's top award ceremonies such as the Loeries.

With this glimpse into the Zimbabwe’s advertising, Charteris will be able to tick another box on the list of African advertising industries he has experienced. It can only help bring fresh insights into the other African markets he operates in, specifically his home country, Tanzania. Charteris has also been invited to return to the Ngomas as the external Judge in the future.
Tunakumbuka vyazi la siku hiyo lilikuwa kufananisha na rangi za bendera ya Tanzania. Waliopendeza walizawadiwa na Amarula.
 Brand manager wa Amarula, Diana Balyagati akiwapa waliofanikisha kushona na kufananisha rangi za bendera ya Taifa.
Hongereni sana wadada na wanawake kwa ujumla kwa kuweka juhudi ya kushona. Asante pia kwa AMARULA kwa kufanikisha.Najua ilikuwa kazi kubwa sana ila mimi  kupitia hii nimepata wazo flani hivi ntawashirikisha muda ukifika.
Ni uzinduzi wa album mbili, zenye mchanganyiko wa nyimbo za kihaya, ZIJULIKANAZO KAMA Vol: 1-YESU NI MWEMA na nyingine ni Vol: 5 -NAKUSHUKURU MUNGU.Ukipata tangazo hili USISITE KUMJULISHA MWINGINE. Ni tarehe. 5/5/2013, katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar Es Salaam.Katika uzinduzi huu watapambwa na waimbaji mahiri wa nyimbo za dini kama:-

Kwaya ya Mt. Kizito- Makubuli, Kwaya ya AIC Chang'ombe
Upendo Nkone, KAKAU Band toka Bukoba. Emmanuel Mugaya "Masanja Mkandamizaji". Kiingilio kitakuwa kama ifuatavyo: Single size ticket (mtu mmoja) -15,000, Family size ticket (Watu 4) -50,000, Special seats (Wa5) 100,000, Watoto 5,000

WATU WOTE MNAKARIBISHWA TUMTUKUZE MUNGU KWA NYIMBO!!
Msanii wa muziki wa taarabu na bongo fleva, Hammer Q akiwa na mkewe ambaye wakati wa harusi yao. Kwa mujibu wa mashuhuda wa habari walisema kuwa kipigo hiki kilitokana mkewe kumtambulisha Hassan Tx Moshi kuwa ni kaka yake ndipo kilipotokea kizaa. Baadhi ya picha za mkewe baada ya kipigooooo.


Mkewe akionyesha alama alizopata baada ya kipigo.


 Nguo za Hammer Q zikiwa zimetapakaa damu hatariiiii.
Baadhi ya ndugu wakiwa wamekusanyika kama msiba maana walijua mke wake amefariki baada ya kipigo kikali. Picha zote kwa hisani ya http://didamitikisiko.blogspot.com

Every day hundreds of thousands of Kenyan schoolgirls head to school to pursue education, with their ambition to become doctors, lawyers and other prestigious occupations. Every evening, they head home to complete their homework and revise their schoolwork. But for some schoolgirls in Mombasa County, every evening brings with it the dark side of their lives, that of forced prostitution and with it the perils of the flesh trade which they claim dire circumstances have forced them into. Lulu Hassan visited Mombasa and brought us that story of "Stolen Innocence".
Msaniii wa Miondoko ya Hip Hop, Roma Mkatoriki akitoa burudani kwa maelfu ya wakazi wa Mwanza waliofurika katika viwanja vya Furahisha Mkoani humo kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha uliofanyika mwishoni mwa wiki kwa siku mbili mfululizo.

Madee akifanya mambo Msanii wa Bongo Flava toka kundi la Tip Top Connection lenye makazi yake mtaa wa Manzese Dar es salaam maarufu kwa jina la Madee akitumbuiza katika tamasha maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha lililofanyika mkoani Mwanza katika viwanja vya Furahisha mwishoni mwa wiki hii.
Msanii Chipukizi aliyeonyesha kipaji cha hali ya juu kwa kughani mashairi yenye mvuto kwa miondoko ya HIPHOP wa mkoani Mwanza maarufu kwa jina la Dogo D alifanya burudani kali katika tamasha maalum la Airtel yatosha mkoani Mwanza katika viwanja vya Furahisha
Wananchi mbalimbali wa mkoani mwanza walijitokeza na kujiuga na Airtel ili waweze kutumia huduma za Airtel Yatosha.
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ameachiwa kwa dhamana hivi punde baada ya kushtakiwa kwa makosa ya uchochezi katika mahakama ya Mkoa wa Arusha huku maandamano yakifanyika hivi sasa katika mitaa ya Jiji la Arusha, Tanzania. Katika Mahakama hiyo kulikuwa na umati mkubwa wa wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mashabiki, wafuasi na wanachama wa chama hicho walifurika katika mahakama hiyo kwa ajili ya kumuunga mkono mbunge huo.
Wafuasi wa Chama cha CHADEMA
Hivi sasa mashabiki, wafurukutwa na wanachama wa Chadema wanafanya maandamano makubwa kuelekea katika ofisi za chama hicho ambazo zipo katika eneo la Ngarenaro.

Hivi sasa wanapita katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mulongo kwa maandamano huku wakipiga kelele za kuzomea. Kesi ya uchochezi dhidi ya Lema imefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Arusha huku ikiendeshwa na Hakimu Devota Msoffe ambapo kesi hiyo imeahirishwa mpaka Mei 29 mwaka huu.

Katika hati ya mashtaka ambayo ipo katika mahakama hiyo inasema kwamba kosa la Lema ni ‘ kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ni uchochezi.

Picha zote na Sillas Mbuya.
Vice President of the European Parliament (EP) Isabelle Durant Sunday said that the freedom of the Palestinian people is urgent and they must be given support in order to achieve it.

Durant told WAFA in an interview that she has been following up on the Palestinian cause for over 20 years and this is the first time for her to visit Palestine.

She said that the Palestinians’ suffering that she witnessed firsthand indicates that it is of utmost importance to help them gain their freedom using nonviolent methods.

Durant, who came to attend the “Freedom and Dignity” conference held in Ramallah to discuss issues related to the Palestinian prisoners and their conditions in Israeli jails, said that this conference was different in that it had a highly innovative, interactive and representative format with the participation, inter alia, of civil society.

On behalf of the EP president, Martin Schulz, Durant attended the conference wishing it to be the beginning of something bigger that could help the Palestinians gain their freedom.

She called for an increasing support to Palestinians within the EP and affirmed that she will be brief its members on all that she heard and saw in order to help the Palestinians gain their freedom and independence.

Durant emphasized that the EP is doing its best to free and protect the prisoners’ dignity “especially when they are being imprisoned without charge or trial.”
Diwani wa kata ya Bulyanhulu Bw. Joseph Makoba akikata utepe kuzindua minara mipya ya kampuni ya simu za mkononi Tigo kata za Kakola na Segese wilayani Kahama mkoani Shinyanga, anayeshuhudia ni meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Bw. Joseph Mutalemwa.
Na Mwandishi wetu.

Tigo Tanzania leo wanaendeleza mipango yao ya kuwekeza katika upanuzi wa mtandao wake katika Kata za Kakola na Segese wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ili kuongeza kiwango cha ubora na upatikanaji wa mtandao huo nchini kote. 

Upanuzi huo pia utakwenda sambamba na kujenga miundombinu mipya ya mawasiliano hasa katika maeneo ya vijijini, kuleta mawasiliano kwa maelfu ya watu. Minara mipya ya mawasiliano itajengwa nchi nzima ambapo mradi huo umeanzia katika mkoa wa Kigoma na kuendelea maeneo kama Mwanza, Tabora, Mara na Kagera.

Akitangaza mradi huo, Meneja Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez alisema “Tigo Tanzania imeendelea kukua kwa kasi mwaka hadi mwaka. Bidhaa zetu za kipekee na huduma pamoja na kuongezeka kwa wateja ni ushahidi wa wazi kabisa wa kukua kwetu. 

Uzinduzi wa minara hii mipya utawezesha kuwapatia wateja wetu bidhaa bora za kipekee zilizobuniwa katika ubora wa hali ya juu ili wateja wetu waweze kunufaika na huduma na bidhaa zenye kiwango cha hali ya juu kabisa kwa hatua mpya. Hii ndio dhamira yetu ambayo imetufanya tuendelee kuwa kampuni inayoongoza ya mtandao wa simu za mkononi Tanzania.”

Tukiwa tayari na mtandao imara wa mawasiliano katika mikoa mingi ya Tanzania bara na Zanzibar, upanuzi huu wa mtandao wetu unalenga kuhakikisha kuwa mtandao wetu unapatikana katika mikoa mingi zaidi nchini. Itaboresha ubora wa mtandao katika maeneo ambayo tayari yana mtandao wa Tigo kuhakikisha mawasiliano yanaboreka zaidi na huduma za Intaneti zinapatikana vizuri zaidi na wakati huo huo kuhakikisha kuwa tunapeleka huduma za mtandao wa Tigo nje kidogo ya Tanzania, kuwawezesha wateja wapya kuungana na wenzao ulimwenguni na kuwa sehemu ya jamii kubwa ya mtandao wa mawasiliano ya simu.

“Tukiwa tunajiamini katika utoaji wa huduma bora za mawasiliano ya simu na nia ya kuendelea kusonga mbele zaidi kwa siku zijazo, tumeona umuhimu wa kupanua na kuboresha mtandao wetu. Uzinduzi wa minara hii mipya utatuwezesha kupanua huduma zetu za mawasiliano katika maeneo haya mapya, kwa wateja tulionao na tutakaokuwa nao kama tunavyodhamiria”

Awali upanuzi wa mtandao wa Tigo vijijini ulianzia kata za wilayani Kasulu mkoani Kigoma

Katika ripoti ya hivi karibuni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya robo mwaka ya mawasiliano ya mwezi Septemba 2012, idadi ya wateja wa Tigo iliongezeka kwa 20% kati ya mwezi Juni mwishoni 2012 na Septemba 30, 2012 ikiwa na wateja 630,000 walioripotiwa. Tukiwa na mikakati hii ya upanuzi, tunatarajia kukua zaidi kwa mwaka huu 2013.
Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamshikilia baba mmoja mkazi wa kijiji cha mkundi katika manispaa ya Morogoro anayefahamika kwa jina la VENANCE MBUA, umri wa miaka 41 kwa kosa la kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka nane.

Akizungumza na waandishi wa habari kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro amesema kuwa baba huyo ambaye aliachana na mke wake na kuishi na watoto wake wawili wakwanza ni wakiume mwenye umri wa miaka 13.

Mtoto huyo ambaye ana majeraha kichwani kwa sasa amefikishwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu pamoja na kupatiwa matibabu.
Imeelezwa kuwa idadi ya wanafunzi wanaomaliza shule Nchini na kushindwa kuendelea na masomo, wanaachwa bila kupatiwa msaada wowote, hivyo wengi wao wakijikuta wanaingia katika lindi la kuwa watoto wa mitaani.

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amebainisha hayo wakati akizindua ofisi ya Kanda ya Magharibi itakayounganisha mikoa mitatu.

Alisema hakuna sera ya kuwasaidia wanafunzi wanaofeli na hivyo kuachwa wakihangaika pasipo msaada wowote.

Awali Naibu Katibu mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, aliwataka wananchi wa Tabora kurudisha heshima ya Mkoa wa Tabora ambao ndio kitovu cha mapambano ya uhuru wa Nchi na kigoma iliyo kitovu cha mapambano ya mageuzi Nchini.

Uzinduzi huo wa Kanda ya Magharibi yenye Mikoa mitatu ya Kigoma, Katavi na Tabora ni kanda ya saba kuzinduliwa Nchini na chama hicho chenye jumla ya kanda kumi lengo likiwa ni kusogeza madaraka kwa wanachama mikoani.
Marais wa jumuiya ya Afrika Mashariki wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka laiyekuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Uganda Marehemu Eriya Kategaya wakati wa ufunguzi wa kikao cha kumi na moja cha Jumuiya hiyo jijini Arusha leo mchan. Katika Hoteli ya Ngurdoto.Kutoka kushoto Rais Wa Burundu Pierre Nkurunzinza,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Marais Wa jumuiya ya Afrika Mashariki waliohudhuria Mkutano wa Wakuu wa jumuiya hiyo katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo.Kutoka kushoto ni Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi,Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda,Mwenyeji wa mkutano Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta. (Picha na Freddy Maro).