Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamshikilia baba mmoja mkazi wa kijiji cha mkundi katika manispaa ya Morogoro anayefahamika kwa jina la VENANCE MBUA, umri wa miaka 41 kwa kosa la kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka nane.

Akizungumza na waandishi wa habari kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro amesema kuwa baba huyo ambaye aliachana na mke wake na kuishi na watoto wake wawili wakwanza ni wakiume mwenye umri wa miaka 13.

Mtoto huyo ambaye ana majeraha kichwani kwa sasa amefikishwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu pamoja na kupatiwa matibabu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: