Imeelezwa kuwa idadi ya wanafunzi wanaomaliza shule Nchini na kushindwa kuendelea na masomo, wanaachwa bila kupatiwa msaada wowote, hivyo wengi wao wakijikuta wanaingia katika lindi la kuwa watoto wa mitaani.
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amebainisha hayo wakati akizindua ofisi ya Kanda ya Magharibi itakayounganisha mikoa mitatu.
Alisema hakuna sera ya kuwasaidia wanafunzi wanaofeli na hivyo kuachwa wakihangaika pasipo msaada wowote.
Awali Naibu Katibu mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, aliwataka wananchi wa Tabora kurudisha heshima ya Mkoa wa Tabora ambao ndio kitovu cha mapambano ya uhuru wa Nchi na kigoma iliyo kitovu cha mapambano ya mageuzi Nchini.
Uzinduzi huo wa Kanda ya Magharibi yenye Mikoa mitatu ya Kigoma, Katavi na Tabora ni kanda ya saba kuzinduliwa Nchini na chama hicho chenye jumla ya kanda kumi lengo likiwa ni kusogeza madaraka kwa wanachama mikoani.



Toa Maoni Yako:
0 comments: