Katika kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika, kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania Limited imetoa mchango wa vitabu, madawati na vifaa vya ujenzi wa madarasa ya shule ambao una thamani ya zaidi ya shillingi milioni 20,000,000 kwa shule zinazohitaji mchango huo mkoani Morogoro.
Akizungumzia kuhusu mchango huo, Meneja wa Mahusiano wa Alliance One, Bw. Hamis Liana, alisema kwamba elimu stahiki kwa Vijana ikiambatana na nyenzo stahiki na mazingira mazuri kwa elimu ni jambo muhimu sana kwa mustakabali wa nchi pamoja na ukuaji na upatikanaji wa viongozi wapya katika miaka 50 ijayo na zaidi ya hapo.
Bw. Mark Mason, Mkurugenzi Mtendaji wa Alliance One aliongezea kwa kusema kwamba mchango huo ni sehemu ya utekelezaji makini pamoja na nia thabiti ya Alliance One ya mpango uwajibikaji wa kibiashara ambao unaunga mkono jamii mbali mbali ambapo kampuni hii inafanya shughuli zake.
Ndani ya mwaka mmoja uliopita pekee, Alliance One ilitoa mchango wa wenye zaidi ya shillingi milioni 40,500.000 wa vifaa vya shule kwenye maeneo ya jamii hizo. Alliance One, kupitia Mpango wa Uwajibikaji wa Kibiashara, inasaidia na kuchangia kwenye maeneo matatu muhimu, ambayo ni afya, elimu na mazingira, ikiwa ni utekelezaji dhahiri wa imani thabiti ya Alliance One kwenye mustakabali wa Tanzania.
Shule ambazo zitanufaika na mchango huo ni Shule ya Sekondari ya Imalamakoye ya Urambo kupitia Chama cha Msingi cha Nsenda; Shule ya Msingi ya Sabasaba ya Morogoro; Shule ya Msingi ya Mitaala ya Kiingereza ya Bernhard Bendel; Shule ya Sekondari ya Kingolwira kupitia Chama cha Msingi cha Msemembo; na mwisho, Shule ya Msingi ya Mahuru Primary School.
Alliance One inaipongeza Tanzania na watu wake ambao wanaadhimisha Miaka 50 ya Uhuru.

Toa Maoni Yako:
0 comments: