Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu STEPHEN WASIRA alirejea msimamo wa serikali ya Tanzania kutokubali sinikizo la nchi ya Uingereza la kuzitaka nchi za Afria kuruhusu ushoga na kuwaomba viongozi wa dini nchini kuungana na serikali kukemea na kulaani kwa nguvu zote ndoa za jinsia moja.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya jubilee ya miaka 50 ya ushirika wa kikristo wa wanafunzi Tanzania –UKWATA, Wasira alisema Tanzania kamwe haitakubali wala kuhalalisha ndoa za jinsi moja licha ya kuendelea kupigiwa kelele na mataifa ya madharibi kwa visingizio vya kuheshimu haki za binadamu.
Maadhimisho ya jubilee ya miaka hamsini ya ushirika wa kikrito wa wanafunzi Tanzania kimefanyika mjini Kibaha mkoani Pwani kikiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na uratibu STEPHEN WASIRA ambapo pamoja na mambo mengine aliwaomba viongozi wa dini nchini kuisaidia serikali kukemea suala lililoibuliwa hivi karibuni na nchi ya Uingereza la kuzitaka nchi zote zinazopewa misaada na Uingereza kuhalalisha vitendo vya ushoga.
Kwa upande wake mlezi wa ushirika wa kikristo wa wanafunzi Tanzania Askofu Godfrey Sehaba alisema pamoja changamoto nyingi zinazoikabili Tanzania wananchi wote wanapaswa kumtegemea Mungu na kuwa wavumilivu
Ibada ya kilele cha maadhimisho ya jubilee ya miaka 50 Ukwata iliandaa sambamba na kusimikwa kwa viongozi wapya Ukwata na uzinduzi wa katiba mpya ya ushirika huo.

Toa Maoni Yako:
0 comments: