Mkuu wa Wilaya ya Singida Paschal Mabiti akimkabidhi vitabu kutoka Tigo, mmoja wa wanafunzi walemavu wa ngozi akisaidiana na Meneja wa kampuni ya Tigo Mkoa wa Singida na Dodoma.
 Mkuu wa Wilaya ya Singida Paschal Mabiti ( wa tatu kutoka kulia) akimkabidhi vitabu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ikungi Oliver Kamily (kushoto). Wengine ni Meneja wa Habari na Mawasiliano, Sylvia Lupembe kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) (wa pili kutoka kulia), Meneja wa kampuni ya Tigo Mkoa wa Singida na Dodoma, Fadhili Saidi (wa kwanza kulia), Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Ikungi, Naftal Gukwi (wa pili kutoka kushoto), Meneja Uhamasishaji Maliasili (TEA), Mr. Charles A. Mapima ( wa tatu kutoka kushoto)
Meneja wa kampuni ya Tigo Mkoa wa Singida na Dodoma, Fadhili Saidi (kushoto) akimkabidhi mwanafunzi mlemavu wa ngozi wa Shule ya Msingi Ikungi mkoa wa Singida , akisaidiana na Meneja wa Habari na Mawasiliano, Sylvia Lupembe kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) –Dar es Salaam (kulia).
---
Katika jitihada za kuendelea kuchangia elimu nchini, kampuni ya simu za mikononi ya Tigo imekabidhi vitabu kwa shule ya msingi ya Ikungi) iliyopo wilayani Singidaa kupitia kampeni yake ya “Tigo tuChange”.

Shule ya msingi ya Toangoma ya jijini DSM ndio iliyofungua mlango wa kampeni ya Tigo tuChange ambapo shule ya msingi Ikungi iliyopokea vitabu hivyo leo hii imekuwa ya nne na zoezi hili litaendelea kwa mikoa ya Mtwara. Tigo lilianza kampeni hii tarehe 9 Septemba ambapo wateja waliweza kuchangia kampeni hii ya Tigo tuChange ndani ya li saa li moja saa tatu mpaka saa nne asubuhi. Tigo iliweza kukusanya fedha taslim ya shillingi 25,930,160 ambazo ndizo zilizotumika kununulia vitabu.

Akielezea madhumuni ya kampeni ya Tigo Tuchange wakati wa kukabidhi vitabu katika shule hiyo, Afisa mauzo wa Tigo, mkoa wa Dodoma na Singida Fadhila Saidi amesema Tigo ni sehemu ya jamii na kwa jamii yoyote ili iweze kuendeleza elimu iliyobora ni nguzo muhimu na kwxa kutambua hilo ndio maana Tigo imeamua kuchangia elimu kupitia vitabu.

Fadhila ameongeza kuwa uzalendo wa watanzania na hasa katika kuipenda Tigo umetoa msukumo wa wao kurudisha sehemu ya faida kwa jamii, ‘watanzania wameendelea kuwa msaada mkubwa kwetu na meendelea kutuunga mkono siku zote sasa na sisi kwanamna ya pekee hasa ukizingatia kuwa Tigo ni sehemu ya watanzania hatuna budi kurudisha sehemu ya kile tunachokipata kwa jamii inayotuunga mkono siku zote.’

Naye mkuu wa wilaya ya Singida Paschal Mabiti amesema amefurahishwa sana na msaada huo ambao umeifikia shule inayoongoza kwa elimu wilayani kwake licha ya uhaba mkubwa wa vitabu unaoikabili na kuzitaka taasisi nyingine binafsi na za serikali kuchangia katika elimu na hasa kuiga mfano huu ambao kampuni ya simu za mkononi ya tigo imeuweka. Kama alivosema afisa uhusiano wa TEA kwamba tunawaomba Tigo kwamba hii isiyo mwisho wa Tigo kutoa msaada katika sekta ya elimu tunategemea kwamba Tigo itaendelea kutoa msaada. Pia tunawahamasisha taasisi na ma kampuni wengine waige mfano ya Tigo Tanzania .

Akiongea kwa niaba ya Mamlaka ya elimu Tanzania TEA, Silvia Lupembe amesema anafurahia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika kusaidia sekta ya elimu. ‘Hatua hii ni nzuri na yenye manufaa kwa Taifa kwani vitabu vimeendelea kuwa tatizo kubwa katika sehemu mbalimbali ndani ya nchi na hivyo tunaishukuru tigo kwa kutufuata na kutaka ushiriki wetu katika kampeni hii na tungependa mashirika na taasisi binafsi na za serikali kuiga mfano huu wa Tigo katika kuchangia elimu ili tuweze kuhakikisha watoto wanapata nyezo muhimu za kujifunzia wakiwa shuleni” .
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: