Wasanii
wa Musiki wa kizazi kipya wa R&B,Hip Hop Belle 9 na
GodZilla,wanatarajiwa kuwa kivutio cha aina yake katika shindano la
kumpata Miss Utalii Dodoma 2011/2012.
Onesho
hilo litakalo fanyika tarehe Jumamosi ya 29-10-2011 katika ukumbi wa
Club La-Azziz Dodoma linataraji kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa
kiserikali wa mjini Dodoma na nje ya Dodoma.
Hii
inatokana na ukweli kwamba kwa muda mrefu kumekuwa na mvutano baina ya
wanamuziki wa kizazi kipya wanao fanya Hip Hop na wale wanao fanya
R& B,kila upande ukidai kuwa aina ya muziki wake iko juu kuliko
nyingine.
Belle
9 anapiga R& B wakati Godzilla anapiga Hip Hop hivyo kufanya usiku
huo wa kumpata Miss Utalii Dodoma 2011/12 kuwa na mvuto na burudani ya
aina yake,kwani pia kutakuwa na burudani ya ngoma za asili kutoka kwa
kundi machachari la ngoma za asili la Yangeyange arts Group la mjini
Dodoma.
Wasanii
hao wa Muziki wa kizazi kipya na wale wa ngoma za asili wamekamiana pia
kuonyesha kipi bora kati ya ngoma za asili na muziki wa kizazi kipya.
Toa Maoni Yako:
0 comments: