Meneja mkuu wa kanda ya kusini Victor Leonard akimkabidhi Rais Jakaya kikwete mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi na saba (17,000,000) ikiwa ni mchango wa Tigo katika kongamano la uwekezaji ukanda wa ziwa Tanganyika.
Meneja mkuu wa kanda ya kusini Victor Leonard akimuelezea Rais juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Tigo kabla ya kumkabidhi rasmi Rais Jaakaya Kikwete mfano wa hundi ya shilingi 17,000,000.
Rais akipewa maelezo na wafanyakazi wa tigo alipotembelea banda la Tigo wakati wa kongamano la uwekezaji ukanda wa ziwa Tanganyika.
Watanzania mbalimbali waliofika katika banda la tigo wakipewa maelezo mbalimbali juu ya huduma za tigo!

---
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imemkabidhi Rais Jakaya kikwete mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi na saba (17,000,000) ikiwa ni mchango wa Tigo katika kongamano la uwekezaji ukanda wa ziwa Tanganyika.
Akiongea katika mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumkabidhi Rais Hundi hiyo Mkuu wa kanda ya kusini Victor Leonard amesema mchango huo unajumuisha pesa taslim shilingi milioni 8.2, Fulana aina ya polo 100, Fulana za shingo ya kuzunguka 200 pamoja na majaketi ya waendesha pikipiki 100.
Victor amesema mchango huo ni kutokana na kampuni ya tigo kutambua umuhimu wa uwekezaji katika maeneo mbalimbali. "Tigo inatambua kuwa kufanikishwa kwa kongamano hili kutaongeza ari ya watanzania wengi zaidi wanaotembelea maeneo haya na kujionea mafanikio ya uwekezaji kufikiria katika kuwekeza katika vitengo mbalimbali vya uchumi na hii itakuwa ni chachu kubwa ya maendeleo kwa watanzania na vilevile kwa taifa zima la Tanzania".
Naye Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kupokea hundi hiyo akaishukuru Tigo na kusema huo ni mfano mzuri na wa kuigwa na makampuni mengine katika jitihada za kupigana na umasikini nakujikuza kiuchumi, Rais Kikwete ameongeza kuwajuhudi zozote zinazoelekezwa katika kusaidia jamii kujikwamua kiuchumi zinaungwa mkono na serikali na kumtaka mkuu wa mkoa wa Rukwa pamoja na mkuu wa wilaya kuimarisha ushirikiano uliopo baina yao na wahisani wanojitolea kwa lengo la maendeleo ya taifa.
Kampuni ya simu z mikononi ya Tigo ndio ilikuwa mdhamini mkuu wa Kongamano hilo kubwa la uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanganyika.

Toa Maoni Yako:
0 comments: