Wakili
Tundu Lisu akitoa maelezo ya mwenendo wa kesi hiyo huku mteja wake
Mbunge Highness Samson (wapili kuia) akimsikiliza kwa makini.
Kesi namba 12/2010 yakupinga matokeo ya uchaguzi mkuu jimbo la ilemela mkoani Mwanza iliyompatia ushindi mbunge kupitia tiketi ya CHADEMA bw. Highness Samson imeahirishwa tena leo jioni katika mahakama ya rufaa jijini humo.
Wakili T. Lisu (kulia) akiwa ameambatana na mteja wake mbunge H. Samson wakitoka kwenye ukumbi wa mahakama.
Kati ya mashitaka tisa yaliyofunguliwa dhidi ya mbunge wa sasa wa Ilemela mashitaka nane yametupiliwa mbali na kubaki shitaka moja tu ambalo ni dai la watu wapatao laki moja na elfu kumi na nne kudaiwa kuzuiwa kupiga kura.

Shitaka
hilo lililosalia linaonekana kukosa nguvu kwani linafananishwa na kesi
ya uchaguzi ya mwaka 1995 ya bw. Silvester Masinde na Pius Msekwa,
ambapo Mahakama ya Rufaa Tanzania iliamuru kuwa kura ambazo hazikupigwa
au hazikuhesabiwa kugawanywa kwa uwiano wa asilimia walizopata wagombea
kwenye uchaguzi.
Mashitaka
nane yaliyofutwa ni pamoja na kufanyika kampeni kwenye vituo vya
kupigia kura na makanisani siku ya kupiga kura, wafuasi wa chadema
kuzuia watu wasipige kura, mgombea wa chadema na mawakala wake kutoa
rushwa kwa kujenga visima kwa wapiga kura na kutoa vinywaji na vyakula
kwenye misiba, mahela yalitolewa kwenye eneo la Manguruwe, mshtakiwa
mbunge pamoja na mawakala wake walinunua shahada za wapiga kura,
kulikuwa na mabadiliko ya vituo vya wapigia kura vituo vya soko la
Kirumba na kwenye viwanja vya Furahisha, jingine ni kuwa kuna mawakala
wa Sangabuye na Buhongwa hawakula kiapo cha kutunza siri.
Mfanyabiashara
maarufu jijini Mwanza Jack Fish' akiteta jambo na mh. mbunge na wakili
wake mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo ambapo inategemewa kusomwa
tena Ijumaa hii 21 oct 2011.
Matokeo
ya uchaguzi huo yanayopingwa ni kuwa Highness Samson aliweza kutangazwa
kuwa mshindi wa kiti cha ubunge wa jimbo la Ilemela kwa kumshinda
Anthony Diallo wa CCM kwa kura 31, 269 dhidi ya kura 26, 270 hii ikiwa ni
tofauti ya kura 4, 999.
Habari na GSengo Blog.
Habari na GSengo Blog.
Toa Maoni Yako:
0 comments: