WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Bulgaria, Nikolay Mladenov amethibitisha kuwa nchi yake iko tayari kuunga mkono juhudi za Palestina kuwa na taifa lake huru.Mladenov alikutana na balozi wa Palestina nchini humo Bwana Ahmed al-Mathbouh, jana katika jitihada za nchi hiyo kukutana mabalozi wa nchi za kiislamu.
Alimweleza juhudi za viongozi wa Palestina za kufufua mazungumzo hayo na nia yao ya kulipeleka suala hilo kwenye Umoja wa Mataifa ili liweze kuungwa kwake mkono kwa uanzishaji wa taifa huru la Palestina.


Toa Maoni Yako:
0 comments: