Ni msichana mcheshi, mwenye sura ya upole na mwenye kupenda watu japo watu wengi humuona ni mwenye maringo na majivuno na huyu si mwingine ni Aneth Kushaba msanii wa bongo flava ambaye aliweza kufanikiwa kuingia katika shindano la Tusker Project la mwaka 2011 na kuitapeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Aneth Kushaba alizaliwa mwaka 1985 siku ya wapendanao namaanisha wengi wao huitambua 'Valentine Day' akiwa ni mtoto wa pili wa mfanyabiashara Mzee Kushaba.
Alisoma shule ya msingi Mgulani JKT jijini Dar es Salaam na baadae akajiunga katika shule ya sekondari Air Wing ya jijini Dar es Salaam na baadae alibahatika na shule ya St. Francis Kampala, Uganda kwa ajili ya masomo yake ya kidato cha tano na sita.
Baada ya kuwa amemaliza huko alirudi nchini na kujiunga na Chuo cha BICO Computer Center.
Aliingia rasmi katika muziki mwaka 2005 kwenye shindano la Gospel Star Search Tanzania ambapo alifanikiwa kuingia katika kumi bora na baadae alikaribishwa kufanya kazi Tanzania House of Talent (T.H.T) kama Volunteer Vocal Trainer mwaka 2006 mpaka 2008. Wakati akiwa T.H.T alifanikiwa kufanya kazi katika band ya B-Band ya Banana, Machozi band, Mjomba Band.
Ilipofika mwaka 2010 aliweza kufanikiwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Tusker Project Fame iliyofanyika nchini Kenya ambapo alifanikiwa kushika nafasi ya 9 katika nchi tano (5) zilizoshiriki.
"Nyimbo za injili ni nzuri na bado nampenda Mungu sana, tuna siri kubwa mimi na yeye uhusiano hauishi, ila kulingana na image nilionayo kwa sasa [Tusker] na jinsi challenge za muziki ulivyo nimeamua kuimba nyimbo za kawaida kwa sababu ya mapenzi yangu na pia kujiongezea kipato," Anasema Aneth.
Mwanadada huyu anakumbuka kuwa wimbo utaomtambulisha na kumuingiza katika humu ulikuwa ukiitwa 'SIKU NAZO' aliotunga mwenyewe kwa kuwaelezea wasichana wenzake kwamba si wanaume wote hawana mapenzi ya kweli ila mpenzi aliyenae yeye ni mkweli na mvumilivu siku zote.
"Mimi ni mwanamuziki kwa sababu najua uwezo nilionao katika muziki na naamini kuwa naweza kufanya vizuri katika industry nikiwa na support nzuri kutoka kwa jamii sababu naweza kuwafurahisha, na mimi ni performer mzuri sana yani mtu hatochoka kunitizama nikiwa naimba kwa stage, i have stage personality," Anasema Aneth huku akitabasamu.
Mbali na muziki Aneth pia ni Afisa masoko katika kampuni ya Utalii na kukodisha magari ya Active tours. Nyimbo ambazo amerekodi mpaka sasa ni Siku Nazo, Weekend Special, Usirudie amezifanyia kwa producer Lamar ndani ya fish crab records, album ambayo ipo katika hatua za mwisho kukamilika.
"Namshukuru Mungu kuwa nyimbo zangu mara nyingi situngiwi hasa hizi za sasa, labda hapo mbeleni nitakapokuwa na mambo mengi nitahitaji mtu anitungie. Jamii naipa kujiamini na kitu wanachofanya, hasa mtu anapoambiwa hawezi jambo kwasababu wakati naingia kwenye muziki nilipata pingamizi sana hasa kwa familia yangu lakini kijiamini na kuonesha kwamba muziki si kitu kibaya au sio uhuni basi wanaweza kukubali kutokana na matendo uyafanyayo, na pia mziki wangu unaelimisha na kuburudisha vijana na wazee.
Akizungumzia mashindano ya tusker project fame Aneth anasema, "Nilikuwa na hamu kushiriki tangu shindano la kwanza lakini nilikuwa sio wakati wangu, mwaka jana wakati naendesha gari kuelekea ofisini nikasikia tangazo Clouds Fm kwakweli nilivutiwa kuingia sababu muda mrefu nilikuwa natamani kukanyaga lile jukwaa na kulitendea haki, na nimefanikiwa kupata exposure katika nchi 5 za Afrika Mashariki na pia hasa kupata urahisi wa kufanya kazi ya muziki kama unavyojua nchi yetu lazima watu wakujue kidogo ili mapokezi ya nyimbo zako iwe ni rahisi.
Anneth anasema kikubwa katika TPF amejifunza jinsi ya kuishi kama mwanamziki japo ni challenge kubwa sana lakini ishaalah ataweza kwa kumshirikisha mwenyezi Mungu. Anasema anahisi imefika wakati watu watakubali kuinvest kwenye muziki, ikiwa ni kujitangaza katika soko la kimataifa kama kwenye festival mbali mbali na vitu kama hivyo, pia wakati tunatunga nyimbo zetu tusiangalie tu kuwafurahisha watanzania hivyo ni kujiwekea wigo wa kazi zetu, wasanii watunge nyimbo huku wakiwaza kuwa watu wa nchi nyingine watafurahi? au ataendana na hisia ya nyimbo hiyo?, tutumie mitandao kama moja ya sehemu ya matangazo yetu, kama twitter, youtube, my space na nyinginezo nyingi ili kufanya mtu wa nchi nyingine kusikiliza nyimbo zetu, nina wanamuziki ambao nawaheshimu hapa kwetu walioweza kuutangaza muziki wetu, utanisamehe sitowataja majina lakini wanatakiwa kuigwa nikiwa mimi mmoja wao naiga nyendo zao.
Akiuzungumzia muziki wa bongo fleva, anasema unachangamoto kubwa sana, kwasababu kuna aina chache sana ya utunzi ambao unaweza kukufanya ufanye za mapenzi nafikiri ndiyo nyimbo zinazouza sana hapa kwetu kwahiyo ili upenye na kutokea vizuri kwenye nyanja hii basi unatakiwa kuumiza kichwa na kufanya kitu chenye hakili kupitia kwa right producers and right camera man, muziki huu hauhitaji kukurupuka hata siku moja.
Kwa sasa mwanadada huyu anatarajia kufanya album ambayo watu wa rika zote watasikiza nyimbo za Aneth, kitaifa na kimataifa pia. Mpaka sasa kwakweli bado sijapata kitu kikubwa cha kuonekana lakini inshaalah mungu mkubwa nitafanikiwa tu, bado nina challenge za hapa na pale lakini naamini ndo ukubwa huo.

big up dada...much respect for you...just make sure u market your album vizuri ili watu tujue....mimi kama mimi lazima ninunue
ReplyDelete