Wazee wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo ilivunjika mwaka 1977 leo hii wamefunga tena barabara ya Kivukoni eneo la Mahakama Kuu kuishinikiza serikali kuwalipa mafao yao wanayodai tangu kuvunjwa kwa jumuiya hiyo.
Wastaafu hao wamesema wanashangazwa na uamuzi uliotolewa na Jaji wa Mahakama hiyo kwamba hawana haki ya kulipwa mafao hao jambo walilolitaja kupingana na agizo alilolitoa Rais Jakaya Kikwete kwamba wastaafu wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki walipwe madai yao.
Machi 15 mwaka huu Rais Jakaya Kikwete aliitaka Wizara ya Fedha na Uchumi kuhakikisha kuwa, kabla ya kuanza mwaka mpya wa fedha wa 2011/12 iwe imelipa madeni yote ya watumishi wa Serikali wakiwamo wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ya zamani.

Toa Maoni Yako:
0 comments: