WATU wawili wamekufa papo hapo na wengine 28 kujeruhiwa vibaya baada ya fuso lenye namba za usajili T115 ANZ walilokuwa wakisafiri kwenda Mnadani Pawaga Iringa kupinduka.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 1 asubuhi leo katika Milima ya umasaini barabara kuu ya Iringa -Pawaga wakati wafanyabiashara hao zaidi ya 50 wakielekea mnadani huku chanzo cha ajali hiyo kikidaiwa kuwa ni uzembe wa dereva ambaye alikuwa akilazimisha kuendesha gari hilo pamoja na kuonyesha matatizo ya bleck kabla ya kuanza kushuka mteremko wa Milima ya umasaini.

Baadhi ya wafanyabiashara walionusurika katika ajali hiyo walimweleza mwandishi wa habari hizi aliyefika eneo la tukio kuwa lori hilo lilianza kusumbua Bleck kabla ya kuanza kushuka mteremko huo hali iliyopelekea dereva na utingo wake kushuka na kujaribu kutengeneza bila mafanikio na kuamua kuliendesha bila bleck ili kuwawahisha wafanyabiashara hao mnadani kwa madai kuwa litafika na kufanyiwa matengenezo mnadani .

Hata hivyo walisema baada ya kuliondoa lori hilo lilianza kushuka kwa kasi kubwa mteremko huo hali iliyopelekea wafanyabiashara kuanza kutaharuki ndani ya lori hilo na baadhi yao kujaribu kuruka kabla ya lori hilo kumshinda dereva huyo na kupinduka .

Abiria hao walisema kuwa dereva huyo alionyesha hofu zaidi baada ya kuona mbele yake kuna karavati la maji machafu na kuamua kulitoa lori hilo nje ya barabara na kupinduka huku likiwa tayari limemaliza mteremko huo.


Kwa upande wake dereva wa lori hilo Wilned Mchala ambaye alikamatwa na kaimu mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa Buzema wakati akijaribu kutoroshwa na mmiliki wa lori hilo baada ya ajali ,alikiri kuwa chanzo cha ajali hiyo ni matatizo ya bleck .

Hata hivyo alisema kuwa hakukuwa na uzembe wowote katika ajali hiyo na kuwa tatizo hilo limetokea ghafla na kuwa pamoja na jitihada kubwa alizozifanya katika kunusuru ajali hiyo ili bado ilionyesha kugonga ukuta.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja waliokufa kuwa ni Jokonia Kihape na Omari Maburuki wote ni wafanyabiashara .

Majeruhi wa ajali hiyo ni pamoja na Vicent Mtewele(20),Stella Nditu(36),John Magubika(45),Chusi Kalinga (22),Evance Ngonyani(31),Wenslaus Njovu(37)Edina Sanga(30),Yassin Alipha(30),Deo Benidict(40) na Ayoub Nzelu(23)

Wengine ni Allen Kisava(22),Erasto Lusungu(25),Emmanuel Mtunye(25),Anthony Kaguo (31),Mengi Kulwa(31),Ally Martine(55),Bony Mwakatebe,Antony Msingi(36),Anania Mkuye(52)

Majeruhi wa ajali hiyo wote wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa huku baadhi yao wakiwa wameumia vibaya kichwani,miguu,mikono na mbavu .


Habari na Francis Godwin kutoka Iringa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: