Wanafunzi wa kidato channe katika shule ya sekondari KIBAHA mkoani Pwani wamegoma kuendelea kufanya mitihani Mock ya kanda ya mashariki inayoendelea kufanyika katika shule zote za sekondari kwa mikoa ya Pwani na Morogoro kwa madai kuwa mitihani sio mipya bali imechukuliwa toka mitihani ya mock ya mwaka jana hivyo haiwezi kuwasaidia kujipima uwezo wao kwani tayari wameshaifanya katika mazoezi ya kila siku darasani.
Wakizungumza na mwandishi wetu mjini Kibaha mara baada ya kutoka katika vyumba vya mitihani wanafunzi hao wamesema wameamua kugoma kuendelea na kitihani hiyo kwa vile imerudiwa hivyo hivyo hawawezi kuwaanda vizuri kwa ajili ya mtihani wa taifa kwavile tayari mitihani yote iliyoletwa ili wafanye walishaifanyia majaribio darasani.
Hawa ni wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Kibaha mkoani Pwani wakitoka darasani baada ya kugoma kuendelea kufanya mitihani ya ya Mock ya kanda ya mashariki kwa kile wanachodai kuwa sio mipya bali imerudiwa toka mitihani ya nyuma hivyo haiwezi kuwaandaa kwa ajili ya kufanya vizuri mtihani wa kumaliza kidato cha nne.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanafunzi hao wamehoji sababu za kuletewa mitihani ambayo imechukuliwa kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka jana bila kubadilishwa hata swali moja ili hali wametoa fedha nyingi kwa ajili ya kugharamia kazi utungaji na usahihisaji wa mtihani hiyi ya mocko.
Kwa upande wao baadhi ya waalimu wanaofundisha shule hiyo wamesema kitendo hicho kinashusha taaluma na hivyo kinaweza kusababisha wanafunzi kushindwa kufanya vyema katika mitihani ya mwisho.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Sekundi Kayenga amekiri kuwa ni kweli wanafunzi wa shule hiyo wamegoma kufanya mtihani na kuthibitidha kuwa ni kweli mitihani hiyo imerudiwa.
Hadi sasa mitihani ambayo imethibitishwa na uongozi wa shule hiyo kuwa imerudiwa ni pamoja na mtihani wa biolojia na somo la kishwahili.

Toa Maoni Yako:
0 comments: