Baadhi ya walimu wa shule za sekondari wilayani ROMBO Mkoani Kilimanjaro wameandamana hadi kwa mkuu wa wilaya hiyo wakidai kutolipwa mishahara yao hali inayowasababishia kuishi maisha magumu.
Walimu hao wamesema kufuatia hali hiyo hawatatunga mitihani ya muhula huu wa sita licha ya kwamba uongozi wa shule wanazotoka umewataka kufanya hivyo.
Walimu hao wamesema wamelazimika kuandamana kutokana na kutolipwa mshahara wao wa mwezi wa nne na kwamba kuandamana ndio njia pekee itakayowawezesha kupatiwa haki yao kwani wamefuatilia suala hilo bila mafanikio yoyote.
Mbali na malalamiko hayo walimu hao pia wamesema mpaka sasa hawaelewi muajiri wao ni yupi kwani wakipeleka malalamiko yao kwa Mkurugenzi au Afisa utumishi wamekuwa wakizungushwa bila mafanikio yoyote.
Akijibu malalamiko hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya ROMBO Samwel Kibaji amesema kilichosababisha walimu hao kutolipwa mishahara yao hadi sasa ni kutokana na baadhi yao kutokamilisha kujaza baadhi ya fomu pamoja na kutopeleka vyeti vyao ili kuthibitishwa na halmashauri
hiyo.

Toa Maoni Yako:
0 comments: