Mkuu wa Mkoa wa Pwani Hajat Amina Said Mrisho amewataka vijana mkoani humo kuwa wabunifu katika kuanzisha shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na kujiongezea kipato na lishe kwa familia kwa kuanzisha bustani za mbogamboga ili kujizalishia ajira kupitia kilimo kidogo.

Akiongea katika uzinduzi rasmi wa mpango wa kazi nje nje ambao unalenga katika kuwawezesha vijana kutambua mbinu mbalimbali zinazoweza kutumika kwa kijana kujitengenezea ajira kulingana na mazingira aliyopo, kwa kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao kwa manufaa yenye kuwawezesha kujipatia kipato,

Ambapo Mkuu huyo ameelezea baadhi ya fursa ambazo mkoa wa Pwani ni pamoja na uwepo wa eneo kubwa la ardhi ambalo halijatumiwa ipasavyo kwa kilimo, na fursa nyingine iliyopo Pwani ni katika sekta ya biashara ambapo kutokana na ongezeko kubwa la watu linalosababishwa na jiji la Dar es Saalam kujaa na kuwafanya baadhi ya wakazi wake kuhamia Mkoani Pwani hasa maeneo ya Mkuranga, Kisarawe, Kibaha na Bagamoyo.

Naye Mwezeshaji kutoka Mpango huo wa kazi nje nje, Bi. Tumusiime Kyando, akisoma risala katika uzinduzi huo ambao unasimamiwa na shirika la kazi Ulimwenguni-ILO- amesema mpango huo maalum wenye lengo la kuwahamasisha vijana na kuwaandaa ili wawe na muelekeo wa kiujasiriamali na waweze kuajirika ama kwa kuajiriwa au kujiajiri na hatimaye waishi maisha ya heshima na kuwa raia wenye manufaa kwa Taifa hili.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: