Walimu watatu wanaume wamesema mimba mashuleni zinachangiwa na wimbi la watu wasio na wito wa taaluma ya ualimu kujiingiza katika kazi hiyo kwa lengo la kupata ajira na kipato kwa urahisi.
Wamesema mwalimu mwenye wito na ambaye amefundishwa maadili ya kazi yake, siku zote hujiheshimu na kujiepusha kuwa na mahusiano mabaya ya kumuharibia maisha wanafunzi wake.
Walimu hao ni Kashushila Shabani, Fredrick Mzirai na Padre Ewald Kilasara wa shule ya secondari ya wasichana ya Mother Teresa of Calcutta iliyoko Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.
Wakizungumza katika mahojiano maalum na waandishi wa TAMWA waliotembelea shule hiyo hivi karibuni walimu hao walisema kuwa kazi ya ualimu inahitaji watu wasio na tamaa ya mali haraka haraka na isiyo halali, wasioendekeza starehe za mwili na ambao wamejengwa vema kiroho.
Walimu hao wameshauri vyuo vya ualimu vizingatie kuwajenga walimu kiroho na kuwapatia stadi za kuwawezesha kuwa na mahusiano mema na wanafunzi kwa ajili ya kuimarisha wanafunzi wao kimasomo na kimaadili.
Wamesema vyuo vya ualimu vitaweza kuwajenga walimu vizuri endapo vitakuwa na wataalamu wa kutosha katika masomo ya sikolojia, sosholojia na filosofia.
Wamesema walimu wenye wito hufanya kazi yao vema na kwa moyo katika kuwajenga wanafunzi kielimu ili waweze kufanya mitihani yao bila hofu, kubabaika au kuibia majibu.
Kadhalika wamesema ni vema shule zote za serikali na za binafsi zikajiwekea sheria na taratibu ambazo zitawawezesha walimu na wanafunzi kutekeleza wajibu wao na kujiepusha na vishawishi vya kuwaingiza katika mahusiano mabaya yanayochangia wanafunzi kufeli masomo au kupata mimba.
Wamesema taratibu hizo ni pamoja na walimu kutoruhusiwa kukutana na wanafunzi nyakati za usiku, makazi ya walimu kuwa mbali na makazi ya wanafunzi na shule kutoruhusu vyakula na vinywaji kuuza hovyo kwa wanafunzi mashuleni.
Walimu hao wamesema shule zikizingatia kuhakikisha kuwa mazingira ya shule yanakuwa salama na bila vishawishi vya aina yoyote kwa wanafunzi na walimu, matukio ya wanafunzi kupata mimba mashuleni na wengine kufeli mitihani yatapungua.
Kwa mujibu wa taarifa za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, katika kipindi cha miaka mitano, 2004-2008, jumla ya wanafunzi 28, 590 wakiwepo 11,599 wa sekondari na 16,991 wa shule za msingi, walikatisha masomo kwa kupata mimba.
Ananilea Nkya
Mkurugenzi Mtendaji

Toa Maoni Yako:
0 comments: