Bingwa wa Olympiki katika mbio za masafa marefu za Marathon Mkenya Samuel Wanjiru (pichani) ameaga dunia.
Duru za polisi zinasema, Wanjiru alikumbana na mauti baada ya kuruka kutoka kwenye chumba chake cha ghorofa moja katika eneo la Nyahururu, huko Kenya.
Idara ya polisi imethibitisha kifo hicho na kusema kwamba uchunguzi umeanzishwa ili kubainisha sababu za kifo hicho.
Mwanariadha huyo alishinda medali ya dhahabu katika mbio za olimpiki mwaka wa 2008 mjini Beijing, kwa kuweka muda wa 2:06:32. na kuandika rekodi ya kuwa mkenya wa kwanza kushinda mbio za marathon kwa upande wa wanaume .
Wanjiru pia alikuwa bingwa wa ulimwengu katika misururu ya mbio za marathon, maarufu kama world marathon majors kuanzia mwaka wa 2008 hadi mwaka wa 2010.
Wanjiru pia aliweka rekodi ya mbio za kilomita 21 kwa kuandika muda wa dakika 58:33.
Mwezi Decemba mwaka uliopita wanjiru alifikishwa mahakama, kwa mashtaka ya kutishia kumuua mkewe, kumjeruhi mlinzi wake wa nyumbani, na pia kumiliki bunduki aina ya AK-47 bila idhini ya serikali.
Mapema mwaka huu Wanjiru alihusika kwenye ajali mbaya katika barabara ya Nairobi kuelekea Nyahururu, hatua iliyomfanya kujiondoa kwenye mbio za London Marathon.

Toa Maoni Yako:
0 comments: