Waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, amesema kufuatia ufaulu wa Masomo ya Sayansi nchini kutoridhisha Serikali inatarajia kuandaa mashindano kwa wanafunzi wanaosoma masomo hayo kwa lengo la kuongeza ushindani zaidi.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Mwaka wa Kimataifa wa Sayansi, Waziri Mbarawa amesema serikali imeazimia kupeleka vifaa maalumu vya kutolea mafunzo kwa njia ya vitendo kwenye shule mbalimbali nchini kwa lengo la kuongeza ufanisi zaidi katika ufundishaji wa masomo hayo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugu, amesema kwa sasa Serikali imeweka kipaumbele zaidi katika masomo ya sayansi kufuatia wanafunzi wengi nchini kuamini kuwa masomo hayo ni magumu na kukimbilia zaidi masomo ya sanaa.

Toa Maoni Yako:
0 comments: