Polisi walimkamata mwanaharakati wa Kimarekani aliyelazwa hospitali baada ya kuingilia kati hotuba ya Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu alipokuwa akihutubia bunge la Marekani.

Mwanaharakati huyo wa miaka 28, Rae Abileah, alisimama bungeni na kupiga kelele “komesheni uharamia wa kijeshi wa Israel” wakati Netanyahu alipokuwa akihutubia.

Abileah, ambaye ni Myahudi wa Kimarekani, alikimbizwa hospitali baada ya kuvamiwa na kuangushwa chini na wanachama wa asasi ya AIPAC. Haya yalisemwa katika taarifa iliyotolewa na NGO iitwayo “Move Over AIPAC”.

Taarifa hiyo ilimnukuu akisema "Nikiwa Myahudi na Mmarekani mlipakodi siwezi kukaa kimya" .

"Netanyahu anasema kuwa mipaka ya 1967 haikubaliki. Lakini kisichokubalika kwa kweli ni uvamizi wa ardhi ya Wapalestina, ukandamizaji wa Gaza, ufungaji jela wa wapinzani na ukosefu wa haki za binadamu," alisema Abileah
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: