RB ya Kituo cha Polisi cha Mabatini, Kijitonyama jijini Dar es Salaam iliyofunguliwa kwa jalada namba KJN/ RB/ 3397 inamsaka mtu anayetajwa kwa jina la Lord Eyez kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Chanzo chetu cha uhakika kimeeleza kuwa, alfajiri ya Jumapili, Mei 22, mwaka huu Lord Eyez anadaiwa kufanya kitendo hicho baada ya kutoka na denti huyo katika ukumbi mmoja wa burudani katikati ya jiji.
Awali Lord Eyez alikodi teksi sambamba na msichana huyo (jina lake linahifadhiwa) aliyekuwa akitaka kurudishwa chuoni kwake IFM. Inadaiwa kuwa, Lord Eyez alitaka kuchangia naye kuchukua teksi hiyo ili kila mmoja apelekwe kwenye maskani yake.
“Lord Eyez alimghiribu denti yule kuwa angekuwa wa kwanza kupelekwa na teski ile hadi chuoni kwake kisha yeye angekuwa wa mwisho,” kilisema chanzo hicho.
Mara baada ya denti huyo kupanda ndani ya teksi, Lord Eyez alimuamrisha dereva kuwapeleka Sinza bila ya kupitia katika Chuo cha IFM kama walivyokubaliana awali.
“Hata yule binti alipokuwa akimhoji dereva kwa nini haanzi kumpeleka chuoni, alimjibu kuwa alikuwa akisikiliza amri kutoka kwa Lord Eyez tu.” Inadaiwa kuwa, wakati wakiwa katika safari ya kwenda Sinza, njiani Lord Eyez aligombana na msichana huyo hadi kumchana na chupa aliyokuwa akimtishia kumkata nayo.
Hata walipofika Sinza Mori, Lord Eyez alihakikisha anamdhibiti denti yule asiweze kufanya fujo.
“Alimchukua hadi chumbani katika nyumba moja ya wageni (gesti bubu) na hata yule demu alipokuwa akisema kuwa yeye si mpenzi wa Lord Eyes hakuna aliyemuamini kwa jinsi alivyokuwa amevaa,” kilisema chanzo chetu.
Inadaiwa kuwa, Lord Eyez alipoingia chumbani na denti huyo alimfanyia vurugu, akamchania nguo yake ya ndani na kumwingilia kwa nguvu.
Denti huyo alipata upenyo wa kuondoka baada ya Lord Eyez kuzidiwa na kilevi alichokitumia kwa kukisokota na kuchanganya na ungaunga uliomfanya kulewa chakari.
Habari kwa hisani ya Global Publisher.
Toa Maoni Yako:
0 comments: