Katika uhusiano wowote wa kimapenzi yafuatayo ni muhimu na bila haya hakuna sababu ya kusema "mnapendana" au kuendelea kuishi/kuwa pamoja.

1.Ushirikiano- Mnahitaji nguzo hii katika nyanja zote yaani kiuchumi, kimwili, kiutendaji (kuanzia shughuli za ndani mpaka zile za chuo/shule), kimawazo n.k.

2.Mawasiliano- Wengi huwa tunazungumza/eleza ikiwa tunafurahishwa tu lakini kukiwa na matatizo au mabadiliko katika uhusiano huwa tunaugulia ndani kwa ndani kitu ambacho si kizuri na kinaweza kuharibu uhusiano wenu. Ni vema kuzungumza wazi na kuhoji kwa upole na upendo ikiwa hufurahishwi na lolote ndani ya uhusiano wako kuanzia utendaji wake kitandani, matumizi ya pesa, wasiwasi n.k. hii itamsaidia kuona tatizo liko wapi na hivyo kushirikiana kulitatua na hivyo kuendeleza penzi lenu.

Heshima- Kutokana na swala la Usawa wa wanawake wengi wamekuwa na viburi. Pamoja na Elimu yako ya juu na mshahara wako mkubwa kuliko yeye heshima inatakiwa kwenye uhusiano wenu ili uwe wenye afya na wa muda mrefu, heshima haishii hapo bali ni kutotoka nje ya uhusiano wenu, kutojiachia na kuonyesha tabia mbovu kama vile kulewa kupita kiasi, kuongea non stop, kuzungumzia maswala ya chumbani, maumbile yake au utendaji wake mbele za rafiki na ndugu zake bila kusahau kukaribisha “shemeji marafiki” nyumbani bila yeye kuwa na taarifa na mwisho kabisa kufanya maamuzi makubwa bila kumuhusisha mwenzio.

Masikilizano na maelewano/makubaliano- Jifunze kusikiliza na kuelewa pale mnapozungumza, si unajua kuna zile “ups na downs seasons”? Kwamba kuna wakati mnafarakana kiaina ndani ya uhusiano na mmoja wenu anasusa/haongei na wewe.

Wanawake wengi wana tabia ya kutolianzisha na akianza basi ni kuingilia mazungumzo kwa vile tu kilichosema kimewagusa (ukweli au uongo) lakini kwa kufanya hivyo hakuna mtu atakaemuelewa mwenzie, hata kama jambo lilikuwa la kawaida tu na kuhakikishia mtaishia kubishana na msifikie muafaka.

Sisemi kuwa ubaki kimya na kuwa “ndio bwana” bali najaribu kusema kuwa ni vema kujifunza kusikiliza na kuelewa kwanza kabla hamjakubaliana na kufikia muafaka kuhusu swala husika.

Kujali- Sote huwa tunaonyesha kujali ikiwa wenza wetu ni wagonjwa, lakini wengi huwa tunajisahau mara baada ya kuwekwa ndani iwe ni kisheria, kidini au kisasa.

Wanawake wengi wana tabia ya kujali watoto wao, marafiki zaidi ya wenza wetu. Vilevile siku hizi kuna hii tekinolojia basi watu twashinda simuni au komputani kuzungumza na marafiki badala ya wapenzi wetu kitu ambacho huwaumiza sana hawa viumbe kihisia lakini kwa vile wameumbwa kuficha hisia zao huwezi kujua, sana sana atachoropoka nje bila wewe kutambua.

Kujali hisia za mwenzako ni muhimu, hivyo kama kuna kitu kinakutatiza au kinakufanya wewe ushindwe kuonyesha hali yakujali kwa mpenzi wako basi rudi kwenye kipengele cha mawasiliano.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: