Pichani ni kushoto ni Meneja wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager, Bw. Allan Chonjo akiwa amepozi na kundi lililoibuka mshindi kwenye shindano la kumsaka mshindi wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta dansi 2011 liitwalo Konte Jazz ndani ya jiji la Arusha, mashindano hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa maraha wa Mawingu Club. Kundi hilo baada ya kujinyakulia ushindi huo kwa kufanya vyema litakutana na makundi mengine kutoka mikoa mingine kadhaa katika kukamilisha kilele cha msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti ndani ya jiji la Dar hapo baadaye.
Kundi la Hot Stone (B-Boyz) wakionysha mbwembwe zao mbele ya mashabiki.

Dj akiwakamulia makundi hayo ya Serengeti Fiesta dansi yalipkuwa yakichuana vilivyo.

Kundi la Konte Jazz likionyesha umahiri wake wa kucheza mbele ya mashaki waliojitokesha kushuhudia shindano hilo ndani ya ukumbi wa Mawingu club, jijini Arusha.

Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kwenye shindano la kumsaka mshindi wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti fiesta dansi,ndani ya Mawingu club, jijini Arusha.


Shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2011 limemalizika leo katika ukumbi wa Mawingu Jijini Arusha leo ambapo kundi la Contegious limeibuka mshindi wa kudance baada ya kuyabwaga makundi mawili ya Hot Stone na The Fuckers yote ya Arusha.

Kutokana na ushindi huo kundi la Contaigous wataungana na makundi mengine kwenye michuano ya fainali ambayo yaliyopatikana Zanzibar, Tanga , huku akali wengine watasaka Mwanza mwishoni na wiki ijayo.

Fainali imepangwa kujumuisha makundi ya kudance kutoka Jijini Dar es Salaam ambapo wamegawanywa katika makundi matatu ambayo ni Kanda ya Ilala, Temeke na Kinondoni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: