Ofisa Uhusiano wa Tigo Tanzania, Jackson Mmbando akizungumza wakati wa promosheni ya huduma ya Tigo Pesa mjini Morogoro mwishoni mwa wiki. Mmoja wa wakazi wa Morogoro, Shadrack Amani akikabidhiwa zawadi ya simu na vocha za Tigo za Sh 50,000/- na Ofisa Uhusiano wa Tigo Tanzania, Jackson Mmbando baada ya kujisajili na huduma ya Tigo Pesa wakati wa promosheni ya humo hiyo mjini humo mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wakazi wa mji wa Morogoro wakijisajili katika huduma ya Tigo Pesa wakati wa promosheni ya huduma hiyo mjini humo mwishoni mwa wiki.
Mpiga besi mahiri wa bendi ya muziki wa dansi ya Akudo Impact, De Kanto na msanii mwingine wa Vijana wa Masauti, Taasisi Masela (kushoto), wakifanya vitu vyao wakati wa onyesho la promosheni ya Tigo Pesa katika Viwanja vya Sabasaba mjini Morogoro mwishoni mwa wiki.

Mwamuziki wa kundi la Tip Top Connection lenye makazi ya mitaa ya Manzese, Dar es Salaam Richard Tunda ‘Tunda Man’ akiwapagaisha wakazi wa mji wa Morogoro wakati wa onyesho la promosheni ya Tigo Pesa katika Viwanja vya Sabasaba mjini Morogoro mwishoni mwa wiki.

Wasanii wa kundi la muziki wa kizazi kipya la Wanaume Halisi, Juma Nature ‘Sir Nature’ (kushoto) na JB ‘Mkuu wa Majeshi’ wakitoa burudani wakati wa onyesho la promosheni ya Tigo Pesa katika Viwanja vya Sabasaba mjini Morogoro mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya wakazi wa mji wa Morogoro waliofurika katika viwanja vya Sabasaba wakati wa onyesho la promosheni ya Tigo Pesa mjini humo mwishoni mwa wiki.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: