muonekano wa barabara ya kwenda kwa mkuu wa mkoa
vijana walioamua kujiajiri kwa kuendesha pikipiki wakisubiri wateja
mwendo wa baiskeli..
biashara ndogo ndogo zinaendelea kama soko la Kariako
Mmezoea Dar kuona wamachinga wanauza vitu vya ndani huku hata kuku wanauzwa katika kati ya mji.Wao bado wapo ulimwengu mwingine hawajui kama kuna mabadiriko.
---
Mkoa wa Tabora upo katika ukanda wa magharibi mwa nchi. Eneo lake ni kilomita za mraba (Km 2 ) 75,264. Kati ya hizo, Km 2 20,637 ni eneo linalofaa kwa kilimo, sawa na asilimia 27.4 ya eneo lote. Eneo la Km 2 54,627 linalobaki ni la misitu, ardhi ya malisho na makazi, mabonde na mbuga, sawa na asilimia 72.6. Mkoa una eneo la ardhi lenye ukubwa wa Hekta 7,526,400 na una eneo la misitu iliyohifadhiwa kisheria kiasi cha Hekta 3,340,000 sawa na asilimia 44 ya eneo lote la Mkoa.

Eneo lenye misitu katika maeneo ya wazi ni hekta 2,792,100 sawa na asilimia 37 ya eneo lote la Mkoa.Uoto wa Mkoa umegawanyika katika kanda za misitu na vichaka, katika ardhi tambarare, mabonde na mbuga zenye majani yanayofaa kwa malisho.Aidha, Mkoa uko katika mwinuko wa kati ya meta 1,100 na 1,300 kutoka usawa wa bahari na hupata mvua ya wastani wa mm 700 – 1,000 kwa mwaka.

UTAWALA: Mkoa una jumla ya Wilaya 6 ambazo ni Nzega , Igunga , Uyui , Sikonge na Urambo zenye Halmashauri za Wilaya na Tabora yenye Halmashauri ya Manispaa. Zaidi ya hapo, Mkoa una Tarafa 19, Kata 135 na Vijiji 525. Aidha, yapo Majimbo ya Uchaguzi 9 ambayo ni Nzega , Bukene, Igunga, Tabora Kaskazini , Igalula, Sikonge , Urambo Magharibi , Urambo Mashariki na Tabora Mjini .

Idadi ya Watu: Mwaka 2002, idadi ya watu Mkoani ilifikia 1,710,465, ambapo kasi ya ongezeko lake kwa mwaka ilikuwa asilimia 3.6, kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2002.

Kwa mwaka huu wa 2010, idadi inakadiriwa kufikia watu 2,349,364 , wanaume 1,151,188 na wanawake 1,198,176 .Asilimia 80 ya wakazi wa Mkoa huu huishi vijijini na hutegemea kilimo, ufugaji na uvunaji wa mazao ya maliasili katika kujipatia riziki yao ya maisha. Asilimia 20 inayoishi mijini hujishughulisha na biashara na kutoa huduma katika Ofisi za umma na katika Sekta Binafsi.

Ukitaka kujua zaidi kuhusu mkoa huu tembelea www.tabora.go.tz
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments: